Michezo

Hii ndio Picha aliyopiga Ronaldo na Bellanova wa AC Millan kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ikimuonyesha Chiellini akiwa uchi

Hii ndio Picha aliyopiga Ronaldo na Bellanova wa AC Millan kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ikimuonyesha Chiellini akiwa uchi

Katika mchezo wa Jumapili hii ambao uliwakutanisha AC Millan ikiwa nyumbani dhidi ya Juventus ambapo Juve walifanikiwa kushinda kwa jumla ya goli 2-0 katika uwanja wa San siro.

Katika mchezo huo Ronaldo alifanikiwa kufunga goli mnamo dakika ya 81 huku goli la kwanza likitiwa kimiani na Mcroatia Mario Mandzukic mnamo dakika ya 8 ya mchezo huo,huku Higuain akipata adhabu ya kutolewa nje ya uwanja baada ya kuonyesha kadi nyekundi baada ya kumchezea rafu Benetia.

Baada ya mchezo huo kumalizika wakati wapo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo Ronaldo aliweza kupiga picha na mchezaji wa AC Milan ambaye pia ni raia wa Ureno Raoul Bellanova ikiwa kama kumbukumbu na katika picha hiyo ilimuonyesha mchezaji wa Juventus Giorgio Chiellini akiwa uchi, Picha hiyo haijaonekana nani aliyeipost ila imeonekana mitandaoni.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents