Habari

Hii ndio ratiba ya serikali kuhamia Dodoma

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Ijumaa hii ametoa ratiba nzima ya serikali kuhamia Dodoma.

imgs3199-1

Ratiba hiyo imetolewa Ijumaa hii wakati Mheshimiwa Majaliwa alipokuwa akiahirisha bunge mjini humo. Uhamaji huo utaanza Septemba mwaka na kumalizika mwaka 2020.

“Awamu ya kwanza itakuwa kuanzia Septemba 2016 mwaka huu hadi Februari, mpaka 2020 watakaohamia ni mheshimiwa waziri mkuu,mawaziri wote,makatibu wakuu wote, na manaibu katibu wote watahamia Dodoma katika awamu ya kwanza,” alisema. “Aidha kila wizara inatakiwa kuwahamisha watumishi wa idara moja au mbili na wakati huo huo wakiendelea kuweka utaratibu mwingine wa idara nyingine kuhamia Dodoma.”

“Awamu ya pili itakuwa Machi 2017 na Agosti 2017. Kipindi hiki kitawapa fursa watendaji wa wizara mbalimbali kuweka bajeti zao za mwaka 2017 na 2018 na kuendelea kuwahamisha watumishi wake kuja Dodoma. Awamu ya tatu itakuwa kati ya Septemba 2017 na Februari 2018, ambapo wizara zitaendelea na uhamishaji wa wa watumishi wa idara zilizo ndani ya wizara zao,” aliongeza.

“Awamu ya nne ni Machi 2018 mpaka Agosti 2018 na awamu ya tano ni Septemba 2018 na Februari 2020. Awamu ya sita ni Machi 2020 na June 2020, itakuwa ni ofisi ya rais ikiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na makamu wa rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watakuwa wanafika Dodoma.”

“Nazishauri wizara zote katika zoezi hili la kuhamia Dodoma ni mfumo wa utunzaji kumbukumbu kwa njia ya mafaili, nashauri wizara zote kuanzisha mfumo wa kutunza kumbukumbu kwa njia ya electronic na sio kuhama na mafaili yote kutoka Dar mpaka Dodoma,” alishauri.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents