Hii ndio sababu ya kufanya mziki aina ya Shaku ambayo asili yake ni Nigeria – S2kizzy

Mtayarishaji wa nyimbo hapa nchini Tanzania S2kizzy ameeleza sababu za kufananishwa aina ya mziki anaoufanya na mziki wa Ki-Nigeria ambao unaitwa Shaku.

S2kizzy alisema hayo baada ya mahojiano na Bongo five kuhusu aina ya mziki anaoufanya kwani umekuwa ukifananishwa na mziki wa Nigeria wa Shaku na kutokea malalamiko kuwa Producer huyo sio mbunifu.

“Hiyo ni aina ya mziki inaoitwa Shaku asili yake ni Nigeria ila mimi nafanya mziki aina ya Trap ambayo asili yake ni Marekani, mara nyingine hautakiwi kufanya aina moja ya mziki,sisi tuliangalia soko la Nigeria ili kupata mashabiki wa huko na pia kupata Kolabo za wasanii wa huku”

Baada ya kuulizwa kuhusu kufananishwa nyimbo ya Chombo ya Rayvanny na nyimbo ya Soco ya Wizkid S2kizzy kwamba ame copy na ku paste alieleza kuwa wao waliangalia hasa wafanye mziki wa aina gani ili kupata mashabiki katika nchini ya Nigeria ila haja copy bali kafanya aina moja ya mziki.

“Unapofanya vitu tofauti tofauti hata wasanii wa nje wanakuona kuwa unaweza na pia ukishikilia kuwa mziki wangu ninaofany ani bora kuliko wa mwingine hilo unakosea sisi tumefanya Shaku ambayo asili yake ni Nigeria lakini imeimbwa Bongofleva.

Producer S2kizzy Amefanya nyimbo nyingi na kali sana miongoni mwa nyimbo alizofanya ni pamoja na Chombo ya Rayvanny,Pochi nene aliyoshirikishwa na Rayvanny,Rudi ya Rich Mavoko dhidi ya Patoranking,Wanaona haya aliyoshirikishwa na Country boy pamoja na Khaligraph vile vile nyimbo ya Hesabu aliyofanya na member wa Weusi Nikki wa pili pamoja na Joh Makini.

 

By Ally Juma.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW