Technology

Hii ndio simu ya kwanza na ya kipekee duniani yenye ukubwa wa ndani wa GB1000 (1-Terabyte)

Kama bado unatumia simu zenye uwezo wa ndani wa GB 8&16  sio mbaya tukisema upo nyuma kidogo ya teknolojia kwani dunia inakwenda kasi sana na masuala ya teknolojia.

Kwa sasa simu yenye uwezo mkubwa wa ndani (Internal Storage) ni iPhone X ambapo inaukubwa wa kuanzia GB 64 hadi 256 .

Ukweli ni kwamba tayari iPhone X imepata mshindani wake naye sio mwingine ni simu aina ya Smartisan R1 simu janja yenye ukubwa wa GB 1000 (1 Terabyte).

Simu hizo zinazotengenezwa nchini China, zimewashangaza watu wengi duniani ambapo licha ya kuwa na ukubwa wa ndani pia zina RAM kubwa ya 8 GB.

Zifa nyingine za simu hiyo ni ukubwa wa Kamera ya mbele yenye Megapixel 24 na kamera mbili za nyuma zenye uwezo wa megapixel 20 na 12. huku kioo cha simu hiyo kikiwa na ukubwa wa nchi 6.17.

Hata hivyo simu hiyo imeboreshwa zaidi kwenye upande wa betri ambapo ina uwezo wa kuchaji betri yake yenye ukubwa wa mAh kwa dakika 30 hadi kujaa chaji, ni kutokana na teknolojia ya kisasa ya Qualcomm’s Quick Charge ya 4+ .

Simu hizo zinakuja na rangi mbili nyeusi na nyeupe na tayari zimeanza kuuzwa jana Mei 17 nchini China na bei zake zinatofautiana kutokana na hitaji lako, kwani kuna matoleo yenye GB 64, 128, 1000.

Kwa simu hiyo Smartsan R1 yenye ukubwa wa GB 1000 (1 Terabyte) na RAM GB 8 inauzwa $1388 sawa na tsh milioni 3, 169,000. Bei za simu nyingine ni kama ifuatavyo

  • 6GB RAM + 64GB – CNY3,499 ($549)
  • 6GB RAM + 128GB – CNY3,999 ($627)
  • 8GB RAM + 128GB – CNY4,499 ($705)

Soma zaidi kuhusu sifa nyingine za simu hiyo kwa lugha ya kichina kupitia kwenye website ya kampuni hiyo ya simu -> smartsan.com

Tazama video ya Review ya simu hiyo hapa chini kwa kuangalia muonekano wake na sifa nyingine (Video by Có Phải Mèo Đâu).

https://youtu.be/0AmVE1bGvbw

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents