Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Hii ndio thamani ya gauni la Meghan Markle alilotupia kwenye Christmas

Kwa sasa Meghan Markle ambaye ni mchumba wa Prince Harry anafahamika kama mmoja wa watu wa familia ya malkia. Je unafahamu thamani ya gauni lake alilotupia katika sikukuu ya Christmas?

Mrembo huyo katika kusherehekea hiyo wiki iliyopita wakati alionekana akiwa amevalia gauni la “Velvet Tay” wakati alipokuwa matembezini akitoka katika kanisa la St Mary Magdalene na mpenzi wake.

Inatajwa kuwa thamani ya gauni hilo ni dola 298 sawa na shilingi milioni 6.68 za Kitanzania.

Kitendo cha Meghan kuvalia vazi hilo kimeonekana kuwavutia kampuni ya Club Monaco ambapo kupitia mtandao wao wa Instagram wameweka picha ya Meghan akiwa na Harry na kuandika, “A very short-term #fbf to Christmas Day when we got a peek at the lovely @meghanmarkle wearing our velvet Tay dress to visit the royal family. đŸ™ŒđŸ».”

Vazi hilo limebuniwa na Jessica Mulroney kutoka Canada na linauzwa mtandaoni kupitia Shopbop.

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW