Uncategorized

Hii ndiyo hoteli ya kwanza anga za juu, itakuchukua siku 12 mpaka kufika huko, Imejengwa kwa ukubwa wa ndege

Kituo cha Aurora hoteli ya kwanza duniani – kwenye mzunguko wa obiti katika anga za juu.

Aurora

Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC, Tangazo rasmi kuhus mpango huo lilitolewa Aprili mwaka jana huko San Jose, California Marekani.

Imejengwa kwa ukubwa wa ndege kubwa ya kibinafsi, itakayoruhusu watalii kupaa maili 200 juu ya ardhi ya dunia, na kupata fursa ya kutupia jicho mandhari ya sayari na muanga wa kaskazini na kusini.

Gharama sio nyepesi: safari hiyo ya siku 12 kwenye kituo cha Aurora inayotarajiwa kufanya ziara ya kwanza yakitalii mwaka 2022, ni ya thamani ya $9.5m kwa mtu mmoja.

Hatahivyo, kampuni hiyo inasema orodha ya watu wanaosubiri safari hiyo ya kitalii inakusanywa miezi 7 kabla ya safari yenyewe.

“Sehemu ya hisia tunayotaka kuwapatia watu ni kujua maisha halisi ya mwana anga za juu yalivyo,” amesema Frank Bunger, muasisi na mkurugenzi mtendaji wa Orion Span, kampuni inayosimamia uidhinishaji wa hoteli hiyo ya Aurora.

“lakini tunatarajia wageni wengi watakuwa wakichungulia nje ya madirisha , na kuwaita kila wanaowajua, na iwapo watachoka, tuna tunachokita ‘holodeck,’ mfumo wa uhaisia unaoonyesha hali ilivyo, na unaweza kufanya chochote unachotaka kufanya mfano kuelea katika anga za juu, kutembea kwenye mwezi na hata kucheza gofu.”

Private companies like SpaceX are still testing their vehicles and not yet sending people into space

Kando na kuweza kuchungulia nyota na sayari ya duni kutoka dirishani. inatarajiwa wageni katika Aurora watajaribu kufanya mambo tofuati katika muda watakaokuwa wakiishi katika hoteli hiyo, kama kujaribu kupanda chakula kama inavyofanywa sasa na maafisa katika ISS.

Wengi katika taaluma ya sayansi wanaona kama hatua isiyoepukika katika maisha ya mwanadamu. Lakini kuna na msemo wa kale, kwamba jihadhari kabla ya hatari; kusema kwamba safari ya raia kwenda katika anga za juu ni kitu kilicho katika kiwango cha msingi, bado haielezi hatua imepigwa kiasi gani.

A few moneyed tourists have been able to pay to visit the International Space Station (Credit: Getty Images)

Kila mmoja anakubali kwamba utalii katika anga za juu ni jambo kubwa: ulianza mnamo 2001 wakati raia wa Marekani Dennis Tito alipolilipa shirika la anga za juu Urusi $20m ili kuzuru kituo cha ISS kilichopo huko. baadhi ya mataifa tayari yameidhinisha msingi katika sekta hiyo katika siku zijazo.

Lakini wataalamu wanasubiri kuona iwapo utalii wa raia katika anga za juu unaweza kutekelezwa na kwa namna gani.

Kilichosalia kubainishwa ni usalama, na viwango vya uhandisi kwa mfumo wa usafiri wa raia katika anga za juu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents