Michezo

Hii ndiyo katiba itakayotumika uchaguzi Simba, TFF yaipa baraka

Baada ya kuzuka kwa sinto fahamu miongoni mwa wanachama wa klabu ya Simba juu ya katiba ipi itumike kati ya zamani na ya sasa kwenye uchaguzi Mkuu ujao hatimaye Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), kupitia Mwenyekiti wake wa kamati ya uchaguzi, Revocatus Kuuli amelitolea ufafanuzi jambo hilo.

Katika mahojiano yake na EFM radio kupitia kipindi chao cha michezo, Kuuli amesema kuwa kama kuna katiba mpya na imeshapitishwa na msajili basi hiyo ndiyo itakayo tumika.

“Mimi ni Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi TFF, kama sishiriki basi nitakuwa na wajibu wa kuangalia uchaguzi,” amesema Kuuli.

Revocatus Kuuli ameongeza “Taarifa niliyonayo mpaka sasa hivi ni kwamba klabu imeshafanya mabadiliko ya katiba na msajili ameshapitisha mabadiliko hayo, kwahiyo kwa vyovyote kama kuna katiba mpya na imeshapitishwa na msajili hiyo ndiyo katiba itakayo tumika.”

“Kama kuna mwanachama anadhani kwamba haki yake imepindishwa au inataka kupuuzwa anahaki ya kuchukua hatua zingine ikiwa ni pamoja na kukata rufaa.”

Klabu ya Simba inaelekea kwenye uchaguzi Novemba 3 mwaka huu wakati zoezi la kuchukua fomu za kugombea nyadhifa mbalimbali ikiwemo uwenyekiti na wajumbe limefungwa rasmi 10/09/2018 ambapo jumla ya fomu 21 zimechukuliwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents