Michezo

Hii ndiyo kauli mpya ya kocha wa Man United baada ya kufungwa na Southampton

Kocha wa Klabu ya Manchester United Louis van Gaal amesema yeye pamoja na kikosi chake wanastahili kubeba lawama na kuzomewa na mashabiki baada ya kufungwa goli 1-0 na timu ya Southampton wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani Old Trafford.

3087D5CC00000578-0-image-a-11_1453674521751

Goli la Southampton lilipachikwa na Charlie Austin dakika ya 87 na hilo ndo goli la ushindi lilikuwa.

Man United ipo katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu England pointi tano nyuma ya Tottenham ambao wako nafasi ya nne na pointi 10 nyuma ya wanao ongoza ligi hiyo timu ya Leicester City.

“Wako sahihi kutuzomea. Siwezi kupinga hilo, niiliuona mchezo”, alisema Van Gaal.

“Kwa mabaya au mazuri bado tunatakiwa kuwa pamoja”, aliongeza mdachi huyo baada ya kikosi chake kupokea kipigo cha sita kwenye msimu huu.

United imefanikiwa kupata pointi 37 kwenye michezo yake 23, ni pointi chache katika historia ya klabu hiyo kwenye ligi ya England ambazo ni pointi tatu nyuma ukilinganisha na kipindi wakati yupo David Moyes msimu wa 2013-2014.

“Tunapambana japo tuna idadi kubwa ya majeruhi”, aliongeza Van Gaal.

Kwenye mchezo wa Jumamosi United ilicheza bila ya Ashley Young ambaye Van Gaal anasema anakabiliwa na majeruhi ya muda mrefu. Pia alimpoteza mlinzi wake Matteo Darmian ambaye alitolewa uwanjani na kupelekwa moja kwa moja hospitali.

Kama beki huyo atakuwa nje ya kikosi, hiyo inamaanisha kikosi cha United kitakuwa hakina beki mzoefu wa pembeni ambaye yuko fit huku Luke Shaw akiwa bado anauguza mguu wake uliovunjika September mwaka jana.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents