Burudani

Hii ndiyo sababu inayomfanya Nicki Minaj kupotea mitandaoni

Nicki Minaj amekuwa kimya kwenye mitandao ya kijamii kwasababu anataka kuifanyia kazi albamu yake ya nne bila usumbufu wowote wa mitandaoni

Vyanzo Vilivyopo karibu na Minaj vinasema kuwa Minaj “ana furaha, ana afya nzuri na si mjamzito,” kulingana na TMZ. Rapa huyo haja posti chochote kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram na Twitter tangu Desemba 30 na watu wake wa karibu wanasema kuwa yote hayo anayafanya ile aweze kutoa albamu nzuri kama ile ya mwaka 2014 Pinkprint.

Wendy Williams alizindua kampeni ya kumtafuta kwa msanii huyo katika programu yake.

Kwa sasa, Minaj amekuwa akienda sana studio na wasanii pamoja na maproducer mbalimbali kama Lil Wayne, Mack Maine, na wengine wengi wa kikundi cha Young Money. Minaj ameahidi kuwa hatajihusisha na mtandao wowote wa kijamii mpaka albamu yake ikamilike.

Video ya mwisho Nicki kuonekana ni ya msanii Quavo ‘She For Keeps’

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents