Michezo

Hii ndo tarehe ya Jose Mourinho kutua Man United?

Habari kuhusiana na kocha Jose Mourinho kujiunga na Manchester United zimerudi tena wiki hii baadhi ya vyombo vya habari vya Ureno na Hispania vimekuwa vikikaririwa vikiripoti kwamba Mourinho tayari amesaini mkataba wa awali kwa ajili ya kutua Old Trafford majira ya kiangazi ya msimu huu.

Jose-Mourinho-United-main

Marca wameandika kuwa Jose Mourinho atakuwa kocha mpya wa Man United kuanzia July 1 2016, licha ya kuwa Marca wameandika stori hiyo kama tetesi, lakini inapata nguvu kutokana na gazeti hilo kuandika stori nyingi zilizoandikwa kama tetesi msimu huu zimekuwa za kweli.

Gazeti la Marca linataja kuwa kama Louis van Gaal akiendelea kufanya vibaya kabla ya msimu huu kumalizika atafukuzwa na nafasi yake kurithiwa kwa muda na Ryan Giggs ambaye ni kocha msaidizi na July 1 Jose Mourinho ndio anatajwa kuwa atakuwa kocha rasmi wa Man United

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents