Habari

Hii ni sababu ukiwa tajiri haimaanishi utakuwa na furaha muda wote

Pengine ule msemo kuwa pesa haiwezi kununua furaha una ukweli zaidi ya hata unavyofikiri.

African American woman counting money in living room

Hii ni kwasababu kuna tafiti nyingi zinazohitimisha kuwa utajiri na furaha si vitu vinavyoendana kama inavyotegemewa. Sababu moja kwa mfano, ni kwamba watu matajiri huonekana kuwa watu wasio na moyo wa ukarimu zaidi. Utafiti mmoja ulibaini baada ya washiriki kupewa $10 na kuambiwa kuwa wanaweza kuitoa sehemu au yote kwa mtu mwingine, wale matajiri walitoa chini kwa asilimia 44.

Kwenye ulimwengu halisi, watafiti wamebaini kuwa watu matajiri hutoa kiasi kidogo ukilinganisha na walichonazo kwa misaada. Matajiri pia ni watu wa kujitenga zaidi – kitu ambacho kina madhara kwenye furaha. Kingine kadri watu watu wanavyokuwa na fedha hupenda uhuru zaidi na kupunguza kujichanganya.

Matokeo kutoka kwenye utafiti wa Notre Dame ni kuwa dalili za ukaribu kama vile kugawa fedha, kujitolea na kuwepo kwaajili ya marafiki zilihusishwa zaidi na furaha. Pia ukarimu ulikuwa na madhara chanya kwa asilimia 93 katika nchini 136.

Hiyo ni kwasababu binadamu huonekana kuwa na furaha zaidi pale tunapojichanganya. Tafiti zinaonesha kuwa hatuwezi kuwa na furaha bila kuwa na walau uhusiano wa karibu wa maana. Kadri tunavyofurahia maisha ya kujichanganya, ndivyo ambavyo tunapata hisia chanya.

Kama umebahatika kuwa tajiri, elewa madhara yaliyothibitishwa kisayansi ya kujitenga.

CHANZO: TIME.COM

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents