Hii ni Top 10 ya watoto wa mastaa Bongo wenye followers wengi Instagram

Kwa sasa umekuwa ni mtindo wa kawaida watu kuwafungulia watoto wao akauti Instagram ili kuwawekea picha zao. Leo ningependa kukuletea top ten ya watoto wa wastaa ambao wapo Instagram, orodha imepangwa kwa kuzingatia idadi ya followers.

1. Tiffah wa Diamond & Zari

Katika akaunti yake watu zaidi ya milioni 1.2 wanamfuata, huku yeye akiwafuata watu watatu tu ambao ni pamoja na wazazi wake, huku akituma picha 819.

2. Cookie wa Aunty Ezekiel & Mose Iyobo

Huyu watu zaidi ya 274,000 wanamfuatilia katika akauti yake, huku yeye akiwafuata watu watu wawili tu ambao ni wazazi wake, ameshatuma picha 206.

3. Nillan wa Diamond & Zari

Watu takribani 200,000 wanamfuatilia, huku yeye akiwafuata watu watatu ambao ni wazazi wake na dada yake (Tiffah) na ameshatuma picha 81.

4. Mali wa Ben Pol

Akaunti yake yenye jina Maliboard ina followers 124k, amefuata watu 99 na kuweka picha 27.

5. Tanzanite wa H Baba & Flora Mvungi

Malkia huyu anafuatwa na watu zaidi ya 77,000 huku yeye akiwafuata watu 62 na ametuma picha 3142.

6. Mozzah wa Aslay

Huyu watu zaidi ya 73,000 wanamfuatilia huku yeye akiwafuata watu wawili tu akiwemo baba yake, hadi sasa ameshatuma picha 93.

7. Amaya wa Alikiba

Watu zaidi ya 35,000 wanamfuatilia, huku yeye akiwafata watu 22, na kutuma picha 129.

8. Kendrick wa Mabeste

Mtoto huyu wa rapa Mabeste anafuatwa na watu zaidi ya 33,000 huku yeye akimfuata mtu mmoja tu ambaye ni mdogo wake (Kaytly), ameshatuma picha 168.

9. Sasha wa Faiza Ally & Mr II ‘Sugu’

Katika akauti yake watu zaidi ya 30,000 wanamfuatilia, yeye hajamfuata mtu hata mmoja na hadi sasa ameshatuma picha 1189.

10. Jaden wa Ray Kigosi & Chuchu Hans

Huyu watu zaidi ya 27,000 wanamfuatilia, huku yeye akiwafuata watu wawili tu ambao ni wazazi wake, na ametuma picha 41.

11. Krish wa Irene Uwoya (Bonus)

Watu takribani 15, 000 wanaomfuta, wakati yeye akiwafuata watu 40 na kutuma picha 27.

Na Peter Akaro
Author Professional: Journalist
Contact: 0755 299596

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW