Michezo

Hii sasa sifa!, Shaban Idd Chilunda atupia nne peke yake, Azam yatinga nusu fainali kiulaini 

Mchezaji wa klabu ya Azam FC, Shaban Idd Chilunda hata baada ya kutupia ‘hat-trick’ hii leo kwenye mchezo wake dhidi ya Rayon Sports hakubweteka dakika 64 ya mchezo huo akapachika goli lake la nne akiwatoa kimasomaso Wanarambaramba hao kwenye dimba la Taifa jijini Dar es salaam.

Mabao hayo manne ya Shaban Idd Chilunda yanamfanya kufikisha humla ya goli saba katika michuano ya mwaka huu na kuongoza katika safu ya wapachikaji mpaka sasa.

Katika michuano ya CECAFA Kagame Cup inayoendelea jijini Dar eslaam, Azam FC wamefanikiwa kukata tiketi ya kuingia nusu fainali na hivyo kuumana na Gor Mahia FC ya nchini Kenya.

Wakati kwa upande wa Simba SC ambayo ilijikatia tiketi hiyo hapo jana inasubiri mshindi wa usiku wa leo kati ya JKU au Singida United .

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents