Uncategorized

Hiki ndicho alichofanyiwa Diego Costa na kaka yake siku ya mwaka mpya

Straika wa Atletico Madrid, DiegoCosta amewaonyesha mashabiki zake kipande cha video ambacho kinamuonyesha akiamshwa na kelele za mafataki yaliyokuwa yamewekwa na kaka yake Jair Costa kwenye kitanda alichokuwa amelala wakati wa mwaka mpya.

Costa ambaye amewahi kushinda taji la Premier League akiwa na Chelsea msimu wa mwaka 2016/17 na kurejea  Atletico mwaka 2017 ambapo alishinda taji la EuropaLeague na timu hiyo ya Hispania.

Costa aliukaribisha mwaka 2019 kwa staili ya haina yake baada ya kuwekewa mafataki hayo kitandani alipokuwa amelala na kujikuta akiamka kwa mshtuko mkubwa.

https://www.instagram.com/p/BsIKVVKhvyr/

Kipande hicho cha video alichorikodiwa na kaka yake aliamua kukiweka kwenye mitandao yake ya kijamii nakusambaa haraka kwa mashabiki zake.

Costa kwa sasa akisumbuliwa na majeraha baada ya kutoka kwenye upasuaji wa kifundo chake cha mguu wa kushoto na kutarajiwa kurejea mwezi Februari.

Hadi kufanyika kwa operesheni hiyo, Costa amekuwa akihangaika Atletico Madrid, huku akiongoza kwa kadi za njano zaidi kuliko idadi ya magoli aliyofunga.

Baada ya kushuka dimbani mara 15, Mbrazili huyo anayeitumikia timu ya taifa ya Hispania anajumla ya mabao manne na kadi saba za njano.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents