Burudani

Hiki ndicho kilichompeleka Nash MC Ujerumani

Msanii mwenye msimamo mkali katika utamaduni wa hip hop, Nash MC yupo nchini Ujerumani katika mji wa Bayreuth ambapo amealikwa katika kongamano la Kiswahili ambako atachambua utamaduni wa hip hop na ushiriki wake katika lugha hiyo.

Taarifa iliyotumwa na Nash MC imesema, nimealikwa katika Kongamano la Kiswahili katika chuo kikuu cha Bayreuth ambalo hufanyika kila mwaka na hili ni Kongamano la 30 mwaka huu. Lakini pia nimepata nafasi ya heshima ya kupiga onesho siku ya Jumamosi ambayo ndio itakua siku rasmi ya kusherehekea miaka 30 ya Kongamano hilo. Baada ya hapo nitashiriki katika mjadala wa mahusiano ya Lugha na Maarifa na hapo nitachambua kuhusu Utamaduni wa Hip Hop na ushirikiano wake na lugha ya Kiswahili katika kuwapa watu maarifa.

Kwa kweli ni hatua kubwa za kimafanikio kwa watu wote wanaopenda maendeleo ya Kiswahili na Utamaduni wa Hip Hop halisi kwa ujumla na sio kwangu tu. Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunichagua katika kuwakilisha Tanzania na Utamaduni wangu wa Hip Hop Ulimwenguni. Ujerumani ni moja kati ya nchi zinazothamini utamaduni wa Afrika lakini ndio nchi iliyo juu katika masuala ya Hip Hop kwa sasa duniani.

Nategemea kuwepo hapa kwa Juma moja na baadae nitarejea Tanzania, kuna mambo mengi ya kuongea na nyie wafuasi wangu ambao mmekua mkitukanwa kutwa kucha kwamba Nash amewapa nini sijui hamumkosoi Nash na mambo kibao lakini haya ndio majibu yake. Nash naamini nachokifanya na naamini rizki anatoa Mungu wala sio Radio au TV. Hip Hop nayohubiri inanipa mwanga na mafanikio lakini yote inachangiwa na uvumilivu na nidhamu kubwa niliyonayo katika kazi yangu. Naungana na mswahili, mpambanaji mwenzangu Vitalis Maembe katika kuwakilisha Taifa.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents