Burudani

Hiki ndicho kilichowapeleka Shaa, AY, Chameleone na wengine Nairobi, wadaiwa kulipwa mkwanja mrefu!

Hivi karibuni wasanii mbalimbali wa Afrika Mashariki wakiwemo Shaa, AY, Jose Chameleone na Maurice Kirya waliungana na wenzao wa Kenya ambao ni pamoja na Nameless, Eric Wainaina na Rabbit walikutana jijini Nairobi Kenya kupika kitu kikubwa.

10788041_846247742062013_1148128589_n

Wasanii hao walikuwa nchini humo kushoot reality TV show inayotarajiwa kuwa gumzo. Chanzo kimoja kimeliambia gazeti la The Star, kuwa ni show ya channel ya Maisha Magic.

Chanzo hicho kimesema gharama za utayarishaji wa show hiyo inaweza kufikia shilingi za Kenya milioni 100 hadi 200. Kilisema wasanii hao watakuwa wamelipwa ujira mnono.

Kama tulivyoandika awali, show hiyo inaweza kuwa ni ile ya kusaka vipaji iitwayo Maisha Superstar.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents