Habari

Hiki ndio chanzo cha kifo Larry King akiwa na miaka 87

Larry King , aliyekuwa mtangazaji wa shirika la utangazaji CCN katika kipindi maarufu cha Larry King Live nchini Marekani amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87.

King aliyejizolea umaarufu kutokana na umahiri wake katika tasnia ya utangazaji, akisifika zaidi kwa uelewa mkubwa wa mambo na maswali yaliyowatikisa aliowahoji alikuwa amelazwa hospitali baada ya kugundulika kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mtoto wake katika ukurasa wake wa Facebook, inaeleza kuwa amefariki leo asubuhi Jumamosi Januari 23, 2021 katika hospitali ya Cedars-Sinai Medical Center Los Angeles nchini Marekani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents