Burudani

Hiki ndio kilichopelekea Nicki Minaj na Cardi B kutaka kudundana kwenye sherehe za Harper’s Bazaar ICONS

Hiki ndio kilichopelekea Nicki Minaj na Cardi B kutaka kudundana kwenye sherehe za Harper’s Bazaar ICONS

Mapper wawili wa kike kutoka Marekani hapa nawazungumzia Belcalis Marlenis Almanzar a.k.a Cardi B pamoja na Onika Tanya Maraj a.k.a Nicki Minaj jana usiku kwenya sherehe za Harper’s Bazaar Icons walisadikika kudundana na kurushiana maneno makali.

Wawili hao amabo waliingia kwenye ugomvi kwa kile kilichosemekana Nicki Minaj kubadili mashairi katika nyimbo waliyoshirikishwa na Migos inayokwenda kwa jina la Motorsport, ambapo ilidaiwa Nicki Minaj aliingiza mistari mwanzo halafu akafuata Cardi B lakini baadaye baada ya kurudi Nicki alipata wasaa wa kuisikiliza mistari ya Cardi B na yeye kugundua kuwa msanii huyo amemfunika hivyo Nicki aliomba kubadili mistari yake katika ngoma hiyo,hapo ndipo mwanzo wa Ugomvi ulipoanzia.

Licha ya wawili hao kuvalishwa nywele na Japan hairstylist lakini hawapatani kabisa na hata wakati video ya wimbo huo inaandaliwa hawakuweza kwenda pamoja.

Lakini walipohojiwa na vyombo vya habari Nicki alidai Cardi B amezungumza uongo kwenye vyombo vya habari ingawa yeye alidai hana ugomvi na Cardi B na alimtakia kila la kheri kujifungua salama wakati huo anaujauzito wa mtoto wake wa sasa hivi.

Jana usiku katika sherehe za Harper’s Bazaar Icons wasanii hao walitaka kudundana katika moja ya sherehe zinzofanyika mwisho wa wiki za maonyesho ya mitindo mjini New York.

Vurugu zilianza pale Nicki Minaj alipowasili kwani Cardi B alikuwa wa kwanza kufika alipoingia Nicki ndio vurugu zilianza hadi kupelekea Cardi B kumrushia viatu Nicki baada ya kuamuliwa.

Chanzo cha Ugomvi kimeelezwa na Cardi B kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusema kuwa ” “Nimewaacha wamesema  mengi ya sh * t slide! Nakuruhusu uendelee kuongea na  uwape uongo juu yangu, . Unawatishia wasanii wengine katika sekta hiyo, na kuwaambia kama watafanya kazi nami nitaacha utaacha kufanya nao kazi! Nakuruhusu kuzungumza sh sh t juu yangu! ”

Lakini pia Cardi B alisikika akilalamika na kumtolea maneno makali Nicki kwamba “kaa mbali na binti yangu”

na huu ndio ujumbe wa Cardi B :- 

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents