Michezo

Hiki ndiyo kiasi cha nauli ya kwenda Zambia kuwashuhudia Simba vs Nkana FC 

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC imetangaza utaratibu kwa wanachama wake, mashabiki na wapenzi wa soka wote wanaotaka kuungana nao kwenda nchini Zambia kwaajili ya kusapoti timu hiyo kwenye mchezo wake wa klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Nkana FC.

Kupitia taarifa yao waliyoitoa hivi punde Simba imesema kuwa utaratibu wa safari nauli ni shilingi laki moja na elfu thelathini (130,000), ikiwa ni kwenda na kurudi kutoka jijini Dar es salaam hadi Kitwe huku safari hiyo ikitarajiwa kuanza siku ya Alhamisi.

Licha ya kuwa na nauli msafiri atalazimika kuwa na hati ya kusafiria inayokidhi matakwa ya kisheria pamoja na hati ya chanjo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents