Habari

Hili ndilo swali la kwanza alilouliza Mama Salma Kikwete bungeni

Hatimaye Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mama Salma Kikwete ameuliza swali bungeni tangu ateuliwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli na kuapishwa leo.

Mama Salma aliuliza, “Je, serikali ina mpango gani wa kuongeza huduma ya TASAF kwa wakazi wa mkoa wa Lindi?

https://youtu.be/XF0AS8bb5RU

Swali hilo lilielekezwa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki ambapo aliweza kujibu:

“Kwanza nimpongeze mheshimiwa mama Salma kwa namna ambavyo amekuwa akifuatilia jamii zaidi na kwa siku ya kwanza tu ameweza kuuliza swali hili. Mheshimiwa spika ukiangalia katika mkoa wa Lindi nikitolea tu mfano Lindi DC, tuko Lindi manispaa, Nachingwea, Luangwa pamoja na maeneo mengine niseme tu tumepokea hoja hii na nimhakikishie mheshimiwa mbunge kwamba kwa sasa tumefikia asilimia 70 tumebakiza asilimia 30 yenye vijiji 5690 na tumepanga kwa mwaka huu wa fedha unaokuja wa mwaka 2017/2018 tutaweza kuangalia Kaya zilizobakia laki tatu, hamsini na tano elfu naamini Lindi pia itakuwa ni moja wapo.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents