Habari

Hili ndio jibu la Ruby kuhusu msanii wa kike anayemsumbua kimuziki Tanzania

Msanii wa kike wa muziki wa Bongo Fleva, Ruby ameamua kuweka wazi kuwa kutokana na uwezo wake wa hali ya juu wa kucheza na sauti kwenye nyimbo zake amedai kuwa haoni msanii ambaye anampa changamoto.

Ruby

Ruby baada ya kuulizwa kwenye kipindi cha Joto la Asubuhi cha E-FM kuwa ni msanii gani wa muziki wa kike hapa Tanzania anayempa changamoto alijibu jibu moja tu kuwa “SIJAONA”

Kwa upande, mwingine Ruby amesema kuwa kwa mwaka 2018 amejipanga kufanya mambo makubwa na kudai kuwa zile tofauti zake na baadhi ya vyombo vya habari ikiwemo kituo cha Radio cha Clouds FM kuwa zimeisha na sasa ni mwendo wa kazi tu.

Kuna peace and love kwa watu ambao mwanzo tulikuwa hatupo ok first of all! second kilichobadilika ni akili yangu imebadilika katika utendaji kazi na jinsi ya kuishi pia na watu tofauti tofauti. Kujitathmini sio mbaya ili atleast ujue umefanya nini na nini hujafanya ili uweze kuaccomplish, ndio kitu ambacho mimi nimefanya, nimejaribu kuangalia kipaji changu kwa undani kinadeserve kuwa sehemu na kina stahili kupita njia gani ili kifike kinakostahili kufika, so nikahitaji kuwa na peace and love kwa kila mtu,“amesema Ruby.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents