Fahamu

Hili ndio tambiko lenye vitendo vya kinyama, wanavyofanyiwa wajane nchini Ghana

Hili ndio tambiko lenye vitendo vya kinyama, wanavyofanyiwa wajane nchini Ghana

Kufiwa na mume au mke ni jambo la kutamausha lakini baadhi ya tamaduni duniani huenda likafanya hali kuwa mbaya zaidi kwa wafiwa – hususani linapokuja suala la chakula.

Katika baadhi ya tamaduni, wachumba wanatengwa wakati wa mlo, wanapigwa marufuku kula vyakula vyenye virutubisho na mara nyingine hata hulazimishwa kushiriki tambiko za kudhalilisha na hatari.

Nchini Ghana, kwa kawaida wafiwa wanaotoka katika jamii maskini ndio huathirika pakubwa.

Licha ya kwamba taifa hilo limejaribu kupiga marufuku matambiko yanayowadhalilisha wajane na kuwadhuru, kwa kutunga sheria.

Lakini bado baadhi yao wananyimwa makusudi vyakula vyenye virutubisho – au kukabiliwa na hali mbaya zaidi.

Kuna tambiko ambazo huhusisha mjane kunywa supu iliyotengenezwa kwa sehemu ya mwili wa marehemu mume wake.

The hair and nails of the deceased are served to the widow.Haki miliki ya pichaKATIE HORWICH
Image captionKatika sehemu kadhaa nchini Ghana wajane hulazimishwa kunywa supu iliyotengenezwa kwa nywele au kucha za marehemu

“Nywele na kucha za mrehemu hutumiwa, mwili huoshwa na maji yaliotumika kuuosha hutumika kutengeneza kinywaji anachostahili mwanamke kunywa,” anasema Fati Abdulai, mkurugenzi wa vuguvugu la wajane na yatima – shirika la misaada lililopo kaskazini mwa Ghana.

Baadhi ya wajane hufanikiwa kujikwamua kutokana na tambiko hizi – lakini wengi wanaishi katika umaskini na hawawezi kufanya hivyo.

Na kwa sababu mali hurudi kwa famili ya marehemu, wakati mume anapofariki, wanawake wegi hupoteza mashamba – labda mpaka watakubali kuolewa na jamaa ya marehemu mumewe.

Inakadiriwa kwamba kote duniani kuna takriban wajane milioni 285, na karibu moja kati ya kumi anaishi katika umaskini.

katika nchi nyingi ujane, hutazamwa kama jambo la aibu – na Umoja wa mataifa unataja unyanyasaji huo wajaane kama aina ya ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu.

Samaki, nyama na mayai marufuku

Katika sehemu kadhaa za dunia unyanyapaa unadhirika kwa wajane hata katika jamii za matajiri.

Kwa mujibu wa Chitrita Banger Gee, mwanahistoria wa chakula kutoka Bengali , katika jamii za Kihindi huko Bengal magharibi, ni hadi miongo kadhaa iliyopita ndio hali imebadilika ambapo wajane kutoka tabaka la matajiri walitakiwa kuomba msamaha kwa vifo vya waume zao.

Walipigwa marufuku kula samaki, nyama, mayai, vitunguu na hata vyakula walivyoinuka wakila alafu ghafla wanakatazwa kuvila,” anasema Gee.

“Suala kuu ni kuondosha urutubisho – kana kwamba mjane amefanya makosa, au ametenda dhambi, na ni lazima atubu – hili hufanyika kwa kuwapokonya chakula.”

Chitrita's mother and grandmotherHaki miliki ya pichaCHITRITA BANGER GEE
Image captionMamake Chitrita Gee, Anita Banerjee na nyanyake Prabhabati Mukerjee

Ni jambo aliloshuhudia Gee akiwa mtoto wakati bibi yake alipofiwa na mumewe.

“Binafsi yalikuwa ni mabadiliko makubwa – aliacha kuvaa nguo za kung’ara na vito na kuishia kuvaa nguo nyeupe tu,” anakumbuka. “Aliacha kula chakula na familia na hakuweza kula vyakula vyote, kutokana na kwamba alipigwa marufuku kula baadhi ya vyakula hivyo.

“lakini alipopika, baadhi ya vyakula vilikuwa vitamu mno.”

Kokote kule duniani wakati mtu anapoomboleza, anahitaji urutubisho na furaha inayoweza kutokana na chakula.

Lakini kumpoteza mpenzi wako ambaye umezoea kula naye chakula huenda ikafanya vigumu baada ya wao kuondoka mjane kula chakula kama kawaida – jambo linaloweza kudhoofisha afya ya mwili na akili.

Utafiti uliofanywa China, Ulaya na Marekani umebaini kuwa miongoni mwa wazee, ujane huhusishwa na lishe duni, na waathirika wengi huishia kukonda au kupunguza uzito wa mwili.

Kwa mujibu wa BBC. Uchunguzi umebaini kwamba wajane na wagane wamo katika hatari ya kufariki katika miaka miwili ya kuondokea na waume au wake zao.

Hii ni athari ya kifo inayofahamika pakubwa, na inadhaniwa huenda sababu inatokana na chakula.

Mwanamke mmoja amewaambia watafiti kwamba wakati mumewe alipofariki, alikuwa hana sababu ya kuamka kutoka kitandani asubuhi.

Alisema kwamba mara nyingine alilala kitandani hadi saa tano au saa tisa mchana na utaratibu wake wa kula ukavurugika.

Basi tunaweza vipi kuwasaida watu wanaoondokewa na waume zao?

Lisa Kolb with her husband ErikHaki miliki ya pichaLISA KOLB
Image captionLisa Kolb na marehemu mumewe Erik Kolb

Lisa Kolb, mwandishi na mpishi anayeishi Washington DC, ana mapendekezo kadhaa. Alimpoteza mumewe Erik katika ajali ya kukwea mlima mwaka mmoja na nusu uliopita baada ya kuoana. walikuwa na umri wa miaka 34 tu wakati huo.

“Mpenzi wako, mnapika pamoja, mnakula pamoja – unapompoteza inakupa hisia ya upweke, na kuishia kukaa jikoni peke yako,”anaeleza.

“Kuleta chakula ni muhimu lakini pia ni muhimu zaidi kuwa na watu. Nadhani watu hufikiria, ni kupika tu kwa haraka, ina maana gani kumualika mtu/ Lakini sio mkaango tu ni fursa ya kuwa miongoni mwa watu na kuhisi kwamba wanakujali”.

Kwahivyo kama hujui umuambie nini mtu aliyefiwa na mumewe anayeomboleza , hatua ndogo tu ya kumpikia, au kumkaribisha mle pamoja chakula, huenda ni hatua nzito unayoweza kuifanya kumsaidia.

Mahojiano haya yalipeperushwa katika makala ya The Food Chain Widowed: Food after losskatika BBC World Service.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents