Habari

Hili ndiyo kabila ambalo Bibi harusi mtarajiwa hulishwa nyama, mafuta ya ng’ombe ili anenepe na kuogeshwa maziwa

Uganda ina makabila 56 na katika makabila hayo, kuna wanyankole lenye tabaka mbili Bahima na Biru, huku Wahima wakiwa ni wafugaji na Biru wakiwa ni wakulima. Leo ninakushirikisha utamaduni wa kabila la Wahima.

Haijalishi una mali nyingine kiasi gani, katika kabila la Wahima utajiri wa mwanaume Muhima, unapimwa kwa wingi wa ngombe zake

Wahima au Bahima kwa utamaduni ni wachungaji na hutembea na ng’ombe zao wakitafuta malisho na inasemekana walitembea hadi kusini Magharibi mwa Uganda walipopata makao.

Ng’ombe ndiyo kitu kinachofananishwa na kabila ya Wahima kwasababu utamaduni wao unatokana na mapenzi yao ya kuwachunga ng’ombe.

Haijalishi una mali nyingine kiasi gani, katika kabila la Wahima utajiri wa mwanaume Mhima, unapimwa kwa wingi wa ngombe zake.

Ukiingia kwenye mji wa Wahima wa Mbarara kusini magharibi mwa Uganda, kitu cha kwanza kinacho kukaribisha ni sanamu ya ng’ombe.

Haijalishi Mhima ana ng’ombe wangapi, atajua kila mmoja kwa jina na hatakubali kupoteza hata mmoja bila kugombana.

Miaka kama 15 iliyopita, ilisemekana kuwa ulipokuwa unapita na gari kwenye maeneo ambayo ng’ombe za Bahima huchungiwa, afadhali ungemgonga mtu lakini usimgonge mnyama huyo kwasababu haungetoka hapo ukiwa hai.

Thamani ya ng’ombe na maziwa kwa bibiharusi wa Mhima.Bibi harusi wa kabila la bahima hulishwa nyama, maziwa na mafuta ya ngombe ili aweze kunenepa na kuwa na mwili nyororoBibi harusi mtarajiwa katika kabila la Wahima hulishwa nyama, maziwa na mafuta ya ngombe ili aweze kunenepa na kuwa na mwili nyororo.

Kwa miaka mingi sana, bidhaa za ng’ombe ndiyo vimekuwa chakula cha wahima. Wanakunywa maziwa kama maji, na hawawezi kula chakula bila mafuta ya ngombe au Eeshabwe ambayo hutengenezwa kwa maziwa pia.

Chakula cha Mhima hakiwezi kukosa walau bidhaa mbili za ng’ombe, ima ni maziwa na mafuta ya ng’ombe, au maziwa na nyama ya ng’ombe au hata bidhaa zote kwa mpigo.

Wiki moja kabla ya kuolewa, bibiharusi huoshwa ndani ya maziwa ya ng’ombe na kuyanywa kila siku kwenye maziwa kila siku na baadaye anapakwa mafuta ya ngombe ili ngozi yao iwe laini.

Bibi harusi mtarajiwa katika kabila la bahima hulishwa nyama, maziwa na mafuta ya ngombe ili aweze kunenepa na kuwa na mwili mwororo.

Unene wa mwili wa mwanamke ndio urembo wake. Mwanamke mwembamba huonesha kuwa familia anapotoka ni maskini sana.

Kana kwamba haitoshi, majina ya baadhi ya wasichana au wanawake katika jamii hii huambatana na sifa na maumbile ya ng’ombe, huku urembo wa mwanamke ukilinganishwa na urembo wa ng’ombe, mfano mwendo wake, macho yake na umbo lake la mwili.

Mwanamke mrembo kwa kabila la Wahima huhusishwa na unywaji wa maziwa… mfano utasikia: Mwanamke yule alikunywa maziwa”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents