Habari

‘Hip Hop ni utamaduni na sio muziki’ – Mansu-Li

Mansu-Li“Jamani Hip Hop sio Kurap tu isipokuwa ni utamaduni ambao unahusisha sanaa za aina mbali mbali na tofauti ikiwa ni pamoja na breakdance, graffiti, Dj, Mc n.k na sio lazima mtu uwe unarap” alisema Mansu-Li.

Mansu-Li


“Jamani Hip Hop sio Kurap tu isipokuwa ni utamaduni ambao unahusisha sanaa za aina mbali mbali na tofauti ikiwa ni pamoja na breakdance, graffiti, Dj, Mc n.k na sio lazima mtu uwe unarap ndio ujione Mwanahip hop, Hip hop ni utamaduni na sio muziki” alisema Mansu-Li.


Akizungumza na mwandishi wa Bongo5 Msanii huyu alidai kuwa Hip hop imepata muelekeo kwani atlist kwa sasa watu wanaweza kujua kuwa kuna muziki wa aina hii san asana watu wazima ambao walikuwa wakiupiga sana vita kipindi cha nyuma.


“Kitendo cha Hip Hop kufahamika kwa watu wazima ni moja kati ya hatua ambazo wanaharakati wanatakiwa kupewa pongezi kwa kuweza kuupenyeza hip hop mpaka kufika ilipofika, sasa kinachotakiwa kwa sasa ni kwamba isieleweke kuwa ni muziki bali washabiki waelewe kuwa Hip hop ni utamaduni” alielezea kijana Huyu ambaye anafanya vizuri katika kurepresent mashiti ya Hip hop kinyama.


Pia Msanii huyu amewaonya wale ambao wanakuwa na fikra za kuwahusisha wasanii wa hip hop na masuala ya ugomvi na ukorofi kama ambavyo wengi wamekuwa wakiamini hivyo “Hip hop inasisitiza sana amani na upendo ukiona watu wanaihusisha na vitendo vya kikorofi ujue hao watakuwa na visa vyao binafsi sema wanakuwa wanaamua kukitumia kivuli cha Hip hop”


Mansu-Li hivi sasa yuko katika hatua za mwisho kukamilisha albam yake ambayo anaifanya taratibu na kwa ufasaha katika studio tofauti za hapa jiji, na pia ameshatoka na mikono kadhaa kama vile ‘kina kirefu, sura ya mchezo na nyingine kibao ambazo ziko njiani.


Bofya hapa kuangalia video ya Kina Kirefu Part 1

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents