Uncategorized

Hisabati za Mwinyi Zahera kutwaa Ubingwa za kwama kwa Mnyama ‘Simba wanaweza kutuzuia’

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa timu pekee inayoweza kuwazuia wao kuchukua ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara ni Simba SC na Azam FC pekee.

Zahera ameyasema hayo wakati alipokuwa akihojiwa na Azam Tv, ambapo ametoa hisabati zake za kimichezo kwamba Simba bado inamechi haija cheza (viporo) alkadhalika na Azam, hivyo kama watashinda watakuwa wamejiongezea pointi.

‘’Wanne na watano wameshakuwa na tofauti ya pointi kubwa karibu 17, wanatakiwa washinde mechi zao zote na sisi tupoteze tano ndiyo wanaweza kutuzibia ubingwa na hao wengine waliyobaki wanaweza kutufunga kwenye mchezo ila siyo ubingwa,’’ amesema Zahera.

Kocha huyo aliyeonyesha mafanikio makubwa ndani ya timu hiyo ameongeza ‘’Mwenye uwezo wa kutuzibia ubingwa ni Simba ana tofauti ya paointi tano, na Azam FC wakiwa na tofauti ya alama saba.

‘’Simba leo wana mechi tano wakishinda zote tuna mshinda na ponti tano, Azam ni ponti saba na ana mechi 19 ni nyingi sana hivyo wanaweza kutuzibia ubingwa.’’

https://www.instagram.com/p/BsGg82ghKlg/

Zahera anatajwa kama kocha ambaye amekiongoza kikosi cha Yanga kwa mafanikio makubwa kwenye ligi baada ya kushinda michezo yake yote 18 pasipo kupoteza hata mmoja toka mwanzo mwa msimu, huku akipata matokeo hayo kwenye kipindi ambacho wachezaji wakilalamika kutolipwa mishahara yao kutokana na ukata wa kifedha unao pitia kwa sasa.

Msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara kwa timu 10 za juu

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents