Burudani

Hisia mseto zaibuka baada ya Bahati kuingia studio na Rayvany!

By  | 

Mashabiki nchini Kenya wiki hii waliamkia na habari za kusisimua. Hii ni baada ya msanii wa gospel kutoka jijini Nairobi kuachia ngoma yake mpya aliyomshirikisha Rayvany wa WCB.

Wafuasi wa Bahati wamefurahi sana na kumsifia kwa kuitengeneza collabo hiyo kwa jina Nikumbushe. Kwa muktadha huu, Bahati ambaye ni hasimu wa jadi wa msanii mwenzake wa gospel Willy Paul Msafi, inaonekana amejibu kwa mapigo ya kisawa ziara ya Willy Paul majuma mawili yaliyopita.

Kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya, wafuasi wa Bahati wamekuwa wakipost picha na kumchekelea Willy Paul ambaye wanateta alienda pale WCB kwa majigambo wala hakutoka na chochote huku mwenzake ambaye ni mkarimu na mpole alinyenyekea na mwishoni akafanikiwa kuingia studio na Raymond.

Hata hivyo upande wa Willy Paul, mashabiki wamekuwa wepesi kumkumbusha Bahati ambaye aliutumia ukurasa wa Facebook mwezi wa January na kuomba msamaha wakenya na mashabiki wake akidai kuwa aliwapotosha kwa kujificha kwenye gospel ila hakuna wimbo hata mmoja wake uliohitimu kumtukuza Mungu.

Na hakuishia hapo, Bahati alisema atajaribu iwezekanavyo kuimba nyimbo za kumtukuza Mungu pekee lakini si za kidunia. Mashabiki wa Willy Paul wamemkashifu vikali Bahati kuwa amekuwa kigeugeu na wala hana msimamo.

Hata hivyo kampeni za kuwakutanisha Diamond, Willy Paul na Bahati zilianza miaka mitatu iliyopita. Huku mtangazaji Willy Tuva wa kituo cha redio cha Citizen nchini Kenya akionekana kuwa katika mstari wa mbele kuhakikisha wasanii hawa wawili yaani Willy Paul na Bahati mmoja wao anafanikiwa kuingia studio na Baba Tee.

Huku juhudi za Tuva zikizidi kupamba moto, aliwahi kufanikiwa kumkutanisha Willy Paul na Diamond mjini Nairobi lakini Diamond alisema yupo tayari kuingia studio nao ila anachoomba ni kuwa nyimbo isiwe ya gospel. Chini hapa nimekusogezea video ambayo Tuva aliwakutanisha Diamond na Willy Paul kwa mara ya kwanza mjini Nairobi.

Makala ya: Changez Ndzai (Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Twitter : ChangezN
Instagram:changez_ndzai

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments