Hispania wafuata nyayo za Ureno na Argentina kwenye hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia

Timu ya taifa ya Uhispania leo imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Dunia la dunia kwa kipigo cha goli 4-3 kwa changamoto ya mikwaju ya penati hii ni baada ya kutoka sare ya 1-1 ndani ya dakika 120.

Urusi wakishangilia kufuzu

Penati za Hispania zimecheza na Pique, Iniesta, Ramos ambao wote wamefunga huku Koke na Iago Aspas wakikosa penati zao.

Urusi hao hawajakosa hata penati moja wameshinda zote nne na kwa matokeo hayo wanafuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo yenye msisimko zaidi duniani.

Hispania sasa inaungana na Argentina na Ureno kwa kutolewa katika hatua ya 16 bora ya kombe la dunia.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW