Habari

Historia fupi ya Mtangazaji wa DW Swahili ya Ujerumani Isacc Gamba kabla ya kifo chake

Historia fupi ya Mtangazaji wa DW Swahili ya Ujerumani Isacc Gamba kabla ya kifo chake

Idhaa ya Kiswahili ya  DW ingali ikiomboleza kifo cha mtangazaji Isaac Muyenjwa Gamba, aliyefariki dunia akiwa nyumbani kwake mjini Bonn. Taarifa za kifo chake zimesababisha mshituko mkubwa sio tu katika jengo la DW bali hata nje ya taasisi hii.

Isaac alijunga na DW mnamo mwaka 2015 akitokea stesheni ya Radio One ya mjini Dar es salaam. Vituo vyengine alikofanya kazi ni Radio Free Afrika na Radio Uhuru. Katika kipindi cha muda mfupi  baada ya kuwasili Bonn alifahamika maeneo mengi ya jiji  kutokana na ucheshi wake na  wepesi wa kufahamiana na watu.

Kikazi  alikuwa mtangazaji mahiri kuanzia kwenye habari, ripoti za matukio duniani hadi michezo.  Tokea DW ilipoanza kutangaza ligi kuu  ya Ujerumani- Bundesliga, Isaac alijiunga na kikosi cha watangazaji wengine kuwapa burudani wasikilizaji wa kabumbu. Pambano la mwisho alilotangaza ni mchuano kati ya Augsburg na Borussia Dortmund. Gamba kama wengi walivyokuwa wakimwita alikuwa maarufu hata nje ya Deutsche Welle.

Kwa mujibu wa DW Swahili, Tangu habari za kifo chake zilipojulikana ,waliomfahamu katika maeneo mbalimbali ya jiji la Bonn wamekuwa wakielezea masikitiko yao, wakishtushwa na taarifa hizo. Alhamisi usiku vijana wa asili tafauti walionekana mitaani wakizungumza kwa huzuni kubwa kuhusu msiba huu.

Kufariki kwake ni pengo kwa Idhaa ya Kiswahili ya DW na waandishi habari na watangazaji wa taasisi hii hapa Ujerumani na Tanzania. Tasnia ya habari imepata pigo kubwa . Kwake Mola tumetoka na kwake tutarejea. Tunaomboleza pamoja na ndugu, jamaa na marafiki walioko kila pembe.  tutamkumbuka daima. Mungu amlaze mahala pema peponi. Ameen..

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents