Tia Kitu. Pata Vituuz!

Historia fupi ya nguli wa R&B, R. Kelly na chanzo cha tuhuma zinazomkabili za kuwarubuni mabinti kingono

Wengi wanamjua kwa jina la R.Kelly lakini jina lake halisi ni Robert Sylvester Kelly, ambaye alizaliwa januari 8 ya mwaka 1967 takribani miaka 52 imepita hadi hivi sasa, katika eneo la Chicago Illinois nchini Marekani.

Ni mwandaaji wa muziki kwa maana ni Producer vile vile ni mwandishi mzuri wa mashairi pia ni muimbaji mzuri wa miondoko ya R&B lakini pia ni mchezaji mzuri wa Basketball ambapo miaka ya nyuma alijaribu kucheza katika timu ya Native of Chicago.

R Kelly alianza kujihusisha na mabo ya muziki miaka ya 1980 na mnamo mwaka 1992 alijiunga na kundi la muziki na miondoko ya R&B la Public Announcement, ambalo lilianzishwa mwaka 1991 hapo hapo Chacogo, Illinois nchini Marekani, ambalo lilikuwa linaundwa na watu kama
R. Kelly
Andre Boykins
Earl Robinson
Ricky Webster
Big Mel
Euclid Gray

Kundi hilo lilifanikiwa kutoa baadhi ya vibao vikali kama vile “She’s got that vibe, Honey Love, Slow dance (Hey mr DJ), Dedicated, Body Bumpin (Ippie Yi-Yo) na Mamacita.

Baada ya kufanya hayo yote mnamo mwaka 1992 R Kelly alitoa album yake akiwa kama Solo YA 12 PLAY, ambayo ilikuwa na nyimbo kali kama :-

No.TitleProducer(s)Length
1.Your Body’s Callin’R. Kelly, Timmy Allen4:39
2.Bump n’ GrindR. Kelly4:17
3.“Homie Lover Friend”R. Kelly, Timmy Allen4:23
4.It Seems Like You’re ReadyR. Kelly5:40
5.“Freak Dat Body”R. Kelly3:45
6.“I Like The Crotch On You”R. Kelly6:38
7.Summer BunniesR. Kelly4:15
8.“For You”R. Kelly5:02
9.“Back To the Hood Of Things”R. Kelly3:53
10.SadieR. Kelly4:31
11.Sex Me Pt 1 & 2R. Kelly11:28
12.“12 Play”R. Kelly, Timmy Allen5:56

 Pi R Kelly aliweza kuwa msanii pekee kucheza Basketball baada ya kusajiliwa mwaka 1997. lakini pia alifanikiwa kuwaandikia nyimbo pia kuproduce nyimbo za wasanii wengi wakiwemo msanii Aaliyah Dana Haughton alimaarufu Aaliyah mwaka 1994 katika album yake ya Age Ain’t Nothing but a Number. 

Mnamo mwaka 1996 alifanikiwa kushiriki katika tuzo za Grammy kwa kumwandikia nguli ya Pop duniani marehemu Michael Jacksn wimbo wa ” You are not alone” huku mwaka 2002 na 2004 R Kelly alifanikiwa kutoa album yake aliyoifanya na Jay-Z na kuweza kutajwa kama mkali wa voco na wasanii kama Nas, Sean Combs, pamoja na mkali The Notorious B.I.G.

Lakini mnamo mwaka 2002 iliweza kumtokea habari mbaya ya kupata kesi ya kuwafanyia vitendo vibaya vya kingono mabinti wadogo 21, kesi inayomuumiza kichwa hadi hivi leo.

Mbali na hilo Recording Industry Association of America (RIAA) liliweza kumtaja R Kelly kuwa ndio msanii aliyefanikiwa kuuza muziki wake nchini Marekani na duniani kote kwa kuuza zaidi ya kopi milioni 40 za album yake.

Mnamo mwaka 2011 R Kelly aliweza kutajwa kuwa ni miongoni mwa wasanii waliofanikiwa zaidi katika sanaa katika miondoko ya R&B kwa zaidi ya miaka 25, lakini pia alifanikiwa kutoa Album 12 akiwa mwenyewe na kufanikiwa kuuza zaidi ya kopi milioni 75 katika kila wimbo duniani kote na kumfanya yeye kuwa ndio msanii wa R&B aliyefanikiwa zaidi kati ya miaka ya 1990 na kufanikiwa kuingia katika orodha ya List of best-selling music artists na kufanikiwa kupewa jina la utani la King of R&B yaani Mfalme wa R&B duniani na mfalme wa Pop-Soul na kufanikiwa kuingia katika orodha ya wasanii wa Billboard katika miondoko ya R&B waliofanikiwa zaidi kwa zaidi ya miaka 25. na kuingia katika historia ya wasanii wa R&B waliofanikiwa.

Mbali na hayo mafanikiwa R. Kelly anamiliki baadhi ya tuzo zikiwemo Guinness World Records,Grammy Award, BET,Soul Train, Billboard, NAACP na The American Music Awards (AMAs).

Kuhusu familia R Kelly ana familia na ana watoto watatu, mke wake Andrea Danyell Kelly ambaye alikuwa dansa alimuoa mwaka 1996 na mnamo mwaka 2006 waliachana.

Mbali na historia hiyo fupi ya mkali R Kelly , mnamo February 3, ya mwaka 2002 ilimtokea habari mbaya ya kurubuni kingono mabinti waliochini ya miaka 18 na video hizo zilisambaa bila kujua chanzo cha kusambaza habri hizo ni nani na zilianza kuonekana katika kituo cha Chicago Sun-Times, ambazo zilitoka siku tano baadaye yaani tarehe 8 mwezi huo februari ya mwaka 2002, hizi habari zilimuumiza sana R.Kelly kwani alitakiwa kwenda kupafomu katika mashindano ya wazi ya Olimpic ambayo yalifanyika hapo nchini Marekani.

Katika moja ya mahojiano aliyoyafanya na kituo cha WMAQ-TV na MTV News, R. Kelly alisema, ” Sio yeye aliyeonekana kwenye video zile” ingawa baadaye mwezi wa sita (June) alikuja kushitakiwa kutokana na kosa hilo, katika video zile ingawa R Kelly alikataa lakini ziliwaonyesha mabinti hao wakifanyiwa vitendo hivyo katika nyumba ya R Kelly. Kelly alikamatwa Januari 2003 kwa mashtaka hayo. Mnamo Machi 2004, mashtaka haya yalipunguzwa kutokana na ukosefu wa sababu inayowezekana ya waraka za utafuta.

Baada ya ucheleweshaji wa tarehe, tarehe 27 Oktoba 2006, kata ya Cook, Illinois kwa kusikilizwa kwa mahakama kabla ya kesi kusogezwa na kuwa tarehe kesi halisi itakuwa Februari 7, 2007.

Siku ya shauri hilo kusikilizwa, mwanasheria wa Kelly aliiambia mahakamani kuwa mteja wake hakuweza kuhudhuria kwa sababu alikuwa amefanyiwa “upasuaji. Alitangaza pia kwamba Kelly akiwa “katika hali nzuri na alitarajiwa kutolewa kutoka hospitali baadaye siku hiyo.” Mwanasheria wa Kelly alisema kwamba Kelly (ambaye hakuwa na hatia) angehudhuria tarehe ya pili ya tarehe 21 Februari 2007. Ilikuwa imetangazwa hapo awali na mahakama kuwa videotape ambayo inadaiwa ilionyesha Kelly kufanya vitendo vya ngono na mwanamke mdogo angeonyeshwa hadharani kama ushahidi katika kesi hiyo. Hata hivyo, kesi hiyo ilikuwa imechelewa kutokana na migogoro juu ya wakati mkanda ulifanywa na kutoa muda wa matibabu kwa muhusika.

Baada ya kuanguka na kusababisha mifupa kuvunjika. Baadaye kesi iliwekwa tarehe ya Septemba 17. Ilichukua muda wa miezi sita. Kesi ilianza rasmi Mei 20 na taarifa za ufunguzi kutoka kwa mashtaka na ulinzi. Baada ya wiki mbili, kesi ya upande wa mashitaka imefungwa mnamo Juni 3 wakati wa ulinzi amefungwa mnamo tarehe 9 Juni. Baada ya siku ya maamuzi, Juni 13, juria la Chicago liligundua Kelly hakuwa na hatia ya makosa yote 14.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW