Tupo Nawe

Historia ya mapenzi yamfanya mume wa boss lady Zari wa Uganda kutoangalia Big Brother, kisa ex wa mkewe ni mshiriki

Msimu wa 8 wa Big Brother Africa ‘The Chase’ unazidi kushika kasi, sio tu kwa washiriki lakini hata kufichua nyeti za chini ya kapeti ambazo kama si Big Brother leo hii huenda nisingekuwa naandika habari hii.

Zari pic

Mume wa mjasiriamali mwenye mafanikio makubwa nchini Uganda Zari aitwaye Ivan Ssemwanga, mara baada ya show ya ufunguzi wa shindano la Big Brother Jumapili (May 26) kuanza, alisema hataangalia Big Brother baada ya kugundua kuwa mpenzi wa zamani wa mkewe Zari , staa wa basketball aitwaye Isaac Lugudde LK4 ambaye ni mwakilishi wa Uganda yuko mjengoni, hivyo ni kama tusi kwake.

Wakati akitazama ufunguzi huo kabla washiriki hawajafahamika, Ivan alimuona mshiriki wa kwanza kupanda kwenye stage, bibie Pokello wa Zimbabwe, ambaye alimchagua mpinzani wa Ivan aitwaye Isaac kama mwanaume wa kuingia naye. Baada ya kitendo hicho Ivan aliamua kuswitch kwenye movie na kutweet “Chillin in ma cinema room watching Temptations by Tyler Perry” akiashiria haangalii tena BBA.

Uhusiano wa Zari na Isaac ulikuja miezi kadhaa iliyopita baada ya Zari na mumewe kuachana kwa muda na baadae walikuja kurudiana.

Siku moja baada ya reality show hiyo inayoendelea huko Afrika Kusini kuanza rasmi, msichana mrembo na tajiri wa nchini Uganda ‘boss lady’ Zari Hussein alionyesha jeuri ya pesa kwa kusema hawezi kushindania $300,000 za Big Brother ambazo hazifikii hata thamani ya moja ya magari anayotumia ambayo ni $ 389,500!! Hey peeps! Huyu manzi anamiliki Lamborghini among others.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW