Habari

Hitaji kubwa la nakala za albam ya ‘Soga za Mzawa’ lamfanya One aanze kuchapisha zingine

Rapper One the Incredible ameamua kufyatua nakala zingine za albam yake, SOGA ZA MZAWA aliyoizundua mwaka jana na kumfanya kuahirisha kutoa albam yake mpya ya RAP(Representing Africa Popote), iliyotakiwa kutoka rasmi November 16 na hivyo kumfanya aisogeze mbele hadi mwezi Juni mwakani baada ya kutengeneza menejimenti mpya.

65250_10201036607223426_1161657368_n

Akiongea na kipengele cha ‘Chumba Cha Sindano’ kupitia kipindi cha ‘Kali za Bomba’ cha kituo cha redio cha Bomba FM 104.0, Mbeya hitmaker huyo wa The Incredible, alifunguka: Nilikuwa nimeacha kufyatua nakala kwa sasa hivi, lakini kuanzia Jumamosi zitaanza kupatikana tena, kwa kifupi ni kwamba albam niliacha kuziprint kama miezi miwili na nusu iliyopita, kutokana na suala la kwamba nilikuwa najaribu kuestablish menejimenti yangu mwenyewe na vilevile kwa sababu nilikuwa nimetoka lebel na kumaliza contract kwa hiyo nilikuwa na suala jipya la kuweka menejimenti mpya na jinsi ya kudistribute kazi zangu kwa hiyo nilikuwa nimestop.”

“Lakini kuanzia Jumamosi ijayo kwenye ile HIP HOP Matching lines nitaanza tena kuziachia albam kama kawaida. Lakini albamu yangu ya RAP itatokwa mwakani mwezi wa 6. Kwa hiyo Tarehe 2 vilevile watu wategemee kuna ngoma mpya nitaachia, ni albamu niliyoizindua mwaka jana SOGA ZA MZAWA, kwa sababu watu wengi walikuwa wamedemand lakini nilikuwa nimeacha kuzisambaza kwa sababu vilevile nilikuwa nahandle na mambo mengine na menejimenti nilikuwa nataka kuweka mpya kwa hiyo ni mambo ambayo yalikuwa yemenikeep busy kwa stahili hiyo.”

Msikilize hapa.

[soundcloud url=”https://api.soundcloud.com/tracks/117578193″ width=”100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents