Burudani

Hivi ndivyo Drake alivyookoa maisha ya kijana aliyetaka kujiua UK

Baada ya Drake kusogeza mbele tarehe ya ziara yake ya ‘Boy Meets World Tour’ katika bara la Ulaya iliyotakiwa kuanza Januari 21 mwaka huu, hatimaye ameanza nayo nchini Uingereza.

Kilichomake headlines akiwa nchini humo ni kujitolea kumsaidia mtu aliyetaka kujiuwa. Polisi wa mjini Manchester waliitwa katika daraja la Mancunian baada ya kijana mmoja kupanda kwenye daraja hilo akiwa na nia ya kujitupa chini ili kujiua.

Drake ambaye alikuwa kwenye foleni akiwa kwenye basi lake la ziara aliomba polisi kama wangeweza kumruhusu kuongea na mtu huyo kama njia ya kuokoa maisha yake.

Baada ya kama masaa mawili hivi aliweza kufanya mazungumzo na kijana huyo aliyeweza kushuka kwenye daraja hilo. Drake kwa sasa yupo London kwaajili ya ziara yake huku akitayarisha album mpya More Life.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents