Michezo

Hivi ndivyo Kichuya na Blagnon walivyoipeleka Simba SC kimataifa

Klabu ya Simba SC jana ilitwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho FA kwa kuifunga Mbao FC goli 2-1 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na kufuzu kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani kwa mara ya kwanza baada ya kukaa kwa miaka minne.

Mshambuliaji wa kimataifa wa klabu ya Simba, Frederic Blagnon

 

Wekundu wa Msimbazi walipata magoli yake mawili kupitia kwa washambuliaji wake Fredrick Blagnon na Shiza Kichuya kwa goli la penati wakati bao la kufutia machozi kwa Mbao FC lilifungwa na Ndaki Robert.

Katika mchezo huo wa fainali timu zote mbili zilicheza kwa nguvu na kujilinda kwa umakini hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika timu hizo zilikuwa hazijafungana.

Kipindi cha pili kila timu ilifanya mabadiliko lakini uamuzi wa Joseph Omog kumtoa Said Ndemla dakika 83 na kuingia Fredrick Blagnon uliokuwa ni habari njema kwa Simba.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alifungia Simba bao la kwanza katika dakika 95, lakini Mbao ilisawazisha dakika 109 kupitia Ndaki.

Wakati mashabiki wakiamini mechi hiyo itakwenda kwenye matuta kunako dakika 116, uamuzi wa utata wa mwamuzi Mohamed Kikumbo ulifaidisha Simba SC kwa kupata penati.

Uamuzi ulisababisha wachezaji wa Mbao kumvaa mwamuzi Kikumbo wakipinga uamuzi huo na kusababisha askari kuingia uwanjani kutuliza ghasia.

Baada ya vurugu hizo mpira uliendelea kwa Kichuya kupiga penati hiyo na kuifungia Simba bao la pili la ushindi na kuamsha shangwe uwanjani hapo.

Awali milango ya Uwanja wa Jamhuri ulifungwa saa 8.00 mchana baada ya majukwaa yote kujaa. Ukikadiriwa kutimiza idadi ya mashabiki 23,000 ikiwa ni idadi iliyotangazwa na shirikisho la soka Tanzania (TFF) na chama cha soka Dodoma (Dorefa).

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents