Burudani

Hivi ndivyo mabondia Mayweather na Pacquiao walivyokutana uwanjani baada ya Pacquiao kuomba pambano lingine na Mayweather (+ Video)

Wanamasumbwi, wawili wakubwa duniani Manny Pacquiao kutoka Ufilipino pamoja na Floyd Mayweather kutoka Marekani, wamekutana katika uwanja wa Basketball.

Mabondia hao wamekutana katika uwanja huo nchini Marekani katika moja ya pambano la mpira wa kikapu mjini Los Angles nchini humo.

Ikumbue kuwa Pacquiao yuko Marekani kwa sababu siku za hivi karibuni siku ya jumapili iliyopita alikuwa na pambano lake dhidi ya Mmarekani Adrien Broner na Pacquiao kushinda kwa points (Unanimous Decision) na kufanikiwa kutetea ubingwa wake wa WBA Welterweight.

Baada ya pamabano hilo Pacquiao alitangaza kuwa anataka pambano lingine na Mayweather baada ya kuchapwa na Mayweather katika pambano lao lililopita.

Baada ya kutangaza hivyo Mayweather hakujibu chochote lakini wakati yuko uwanjani akiangalia mchezo wa Basketball alikutana na Pacquiao na kuweza kuslimiana nae.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents