Michezo

Hivi ndivyo matokeo ya mechi za leo yalivyo badili msimamo mzima wa VPL

Ligi kuu soka Tanzania Bara imeendelea tena hii leo kwa michezo miwili kupigwa katika viwanja tofauti.

Kikosi cha Mtibwa Sugar kimekubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Ruvu Shooting katika dimba la Manungu wakati Tanzania Prisons ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Kwa matokeo hayo Tanzania Prisons imepanda hadi nafasi ya tano ikiishusha Mtibwa Sugar, huku Ruvu Shooting ‘Wazee wa kupapasa’ wakizidi kuchanja mbunga hadi namba saba.

Michezo iliyosalia kukamilisha raundi hii ni vinara wa ligi hiyo timu ya Simba dhidi ya Mbao wakati Ndanda ikiwa na kibarua kizito cha kuivaa Yanga SC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents