Michezo

Hivi ndivyo Neymar alivyowanyoosha Juventus (+Video)

Mshambuliaji wa Klabu ya Barcelona ya Hispania, Neymar Jr ameendelea kuudhihirishia ulimwengu kuwa yeye ndiye mchezaji bora kwa sasa kwa kutupia magoli mawili dhidi ya Juventus asubuhi ya leo.

Neymar akiwatoka mabeki wa Juventus

Mchezo huo ambao ulikuwa unasubiriwa na mamilioni ya watu kutazamwa wengi wakimsubiri Neymar kuonesha uwezo wake baada ya tetesi za kuachana na klabu hiyo kuenea, alianza kutupia kunako dakika ya 14 na 25 za kipindi cha kwanza na mpaka mapumziko Barca walikuwa mbele ya goli 2-0 dhidi ya Juventus.
https://youtu.be/BIVkaB7M6oU
Kunako dakika ya 62 kipindi cha pili Juventus walipata goli moja la kufutia machozi na mpaka kipenga cha mwisho Barca 2, Juventus 1.

Mchezo mwingine ulikuwa kati ya PSG dhidi ya Tottenham Hotspurs ambapo uliisha kwa, Matajiri wa Ufaransa PSG kuchabangwa goli 4-2, Michuano ya ‘International Champion Cup’ inayofanyika nchini Marekani itaendelea leo usiku ambapo Miamba wa Uhispania Real Madrid watavaana na Manchester United.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents