Michezo

Hivi ndivyo Rais wa Liberia George Weah alivyoistaafisha Jezi yake katika mtanange huu

Hivi ndivyo Rais wa Liberia George Weah alivyoistaafisha Jezi yake katika mtanange huu

George Tawlon Manneh Oppong Ousman Weah alimaarufu George Weah Rais wa 25 katika taifa la Liberia,katika karia yake aliwahi kucheza mpira wa kimataifa ambapo alivitumikia zaidi ya vilabu 12 barani Afrika pia barani Ulaya.

Weah ndio mchezaji pekee kutoka katika bara la Afrika kuwahi kushinda tuzo ya mwanasoka bora duniani alimaarufu Ballon d’or mnamo mwaka 1995 wakati anaitumikia klabu ya AC Milan.

Licha ya kushinda tuzo hiyo lakini pia amewahi kutwaa tuzo ya mwanasoka bora barani Afrika zaidi ya mara mbili ambapo ni mwaka 1989, 1994, 1995.

George Weah ingawa alifanikiwa kupata mafanikio makubwa kwenye soka lakini hakuweza kulisaidia taifa lake kushinda kombe la mataifa barani Afrika licha ya kuifungia magoli 22 katika michezo 61 kuanzia mwaka 1987 hadi mwaka 2007.

Licha ya kuvaa zaidi namba za jezi zaidi ya tatu katika vilabu vyake alivyovitumikia ikiwa ni jezi namba 9,jezi namba 10,jezi namba 14 jezi namba 22,jezi namba 29 na jezi namba 31,katika timu yake ya taifa aliitumikia jezi namba alitumia jezi namba 14 na katika mchezo wa jana alifanikiwa kucheza mchezo maalumu kwa ajili ya kustaafisha namba ya jezi yake akiwa kama Rais kwa sasa.

na hii ni miongoni mwa faulu aliyoicheza katika mchezo huo.

 

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents