Burudani

Hivi ndivyo Tigo Fiesta, Wasafi Festival na Alikiba watakavyoitikisa Tanzania Novemba 24

Kwa wapenzi wa burudani nchini Tanzania, Jumamosi hii ya Novemba 24, 2018 kutakuwa na matamasha makubwa matatu ya burudani yatakayofanyika mikoa mitatu tofauti.

Image result for tigo fiesta 2018

Tamasha kubwa la kwanza ni lile la fainali ya tamasha la Tigo Fiesta ambalo litafanyika Dar Es Salaam, Fiesta ndio tamasha kubwa la burudani kwa muda wote hapa nchini Tanzania.

Fainali hiyo, itafanyika ikiwa tayari tamasha hilo limeshafanyika karibia mikoa 10 ya Tanzania bara. Hata hivyo bado idadi rasmi ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo hawajatajwa.

Tamasha la pili siku hiyo, ni lile la ufunguzi wa Wasafi Festival mjini Mtwara, Wasafi Festival hii itakuwa ndio safari yao ya kwanza kwenye tasnia lakini kutokana na ukubwa wa maandalizi na promo kutoka kwa Mwanzilishi wa Tamasha hilo, Diamond Platnumz watu wengi wameonekana kuvutiwa na uzinduzi huo.

Tayari majina makubwa ya wasanii kama Harmonize, Mbosso, Rayvanny na wengine kama Nikki Mbishi, Moni Centrozone, Country Boy na wengineo wameshatangaza kuhudhuria.

Tukio lingine la kiburudani siku hiyo, ni show ya Alikiba ambayo itafanyika Kahama, hii ni maalumu kwa mashabiki wake wa  kanda ya ziwa.

Watu wengi hawaiongelei Show ya Alikiba kutokana na mapokeo makubwa ya Tamasha la Wasafi Festival na Fainali ya Tigo Fiesta, lakini hakuna ubishi kuwa show ya Alikiba itawatikisa wakazi wa Kanda ya ziwa.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents