Hivi ndivyo viwanja 12 vitakavyotumika kombe la dunia 2018 Urusi
Wakati mataifa mbalimbali yakijiandaa na michuano ya kombe la dunia linalotarajiwa kufanyika nchini Urusi hapo mwakani tayari viwanja 12, vinatarajiwa kutumika katika mashindano hayo.
Na hivi ndivyo viwanja vitakavotumika katika michuano hiyo mikubwa nay a kwanza kwa ukubwa katika mchezo wa soka.
- Kiwanja kikubwa zaidi katika michuano hiyo nchini Urusi ni Luzhniki kinauwezo wa kuingiza watu 81,000 kitafunguliwa mwakani kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.
Luzhniki Stadium, Moscow
Kinaingiza watu: 81,006
Kilifunguliwa: 1956 (Nakufanyiwa marekebisho na kutarajiwa kufunguliwa 2018)
Hali ya hewa: Kiwango cha juu cha joto ni 23C na cha chini 18C , uwezekano wa kunyesha mvua ni 50%
- Dimba la Spartak ni miongoni mwa viwanja vitakavyotumika kombe la dunia jina hili limebadilishwa katika kipindi hiki cha maandalizi ya michuano hiyo aawali ulikuwa ukiitwa Otkrytiye Arena unauwezo kuingiza watu 43,298.
Spartak Stadium, Moscow
Kinaingiza watu: 43,298
Kilifunguliwa: 2014
Hali ya hewa: Kiwango cha juu cha joto ni 23C na cha chini 18C , uwezekano wa kunyesha mvua ni 50%
- Uwanja huu wa Nizhegorod u[po umbali wa maili 265 mashariki mwa jiji la Moscow eneo lake huvutia hasa kutokana na kuzungwa na viitu vya asili na umbile lake ni duara huku ukiwa na taa kwa nyakati za usiku na unaingiza watu 45,331.
Nizhny Novgorod Stadium, Nizhny Novgorod
Kinaingiza watu: 45,331
Kilifunguliwa: 2018
Hali ya hewa: Kiwango cha juu cha joto ni 23C na cha chini 13C , uwezekano wa kunyesha mvua ni 60%
- Uwanja huu wa Saransk upo Kusini Mashariki mwa jiji la Moscow, Mordovia Arena utakuwa wenye rangi nyingi na za kuvutia kwaajili ya kombe la dunia 2018 na utaingiza watu 45,000.
Mordovia Arena, Saransk
Kinaingiza watu: 45,000
Kilifunguliwa: 2018
Hali ya hewa: Kiwango cha juu cha joto ni 23C na cha chini 12C , uwezekano wa kunyesha mvua ni 33%
- Uwanja wa Kazan Arena unafananishwa na vile vya Wembley na Arsenal wa Emirates. Uwezo wake ni kuingiza watu 45,000
Kazan Arena, Kazan
Kinaingiza watu: 45,000
Kilifunguliwa: 2013
Hali ya hewa: Kiwango cha juu cha joto ni 24C na cha chini 14C , uwezekano wa kunyesha mvua ni 55%
6. Uwanja huu wa Samara bado nao upo katika matengenezo ipo umbali wa maili 655 kutoka jiji la Moscow
Samara Arena, Samara
Kinaingiza watu: 44,807
Kilifunguliwa: 2018
Hali ya hewa: Kiwango cha juu cha joto ni 26C na cha chini 16C , uwezekano wa kunyesha mvua ni 50%
- Kiwanja hiki cha Ekaterinburg kipo katika jiji ambalo ni la nne kwa ukubwa kutokana na ‘geographical’ ya nchi hiyo.
Ekaterinburg Arena, Ekaterinburg
Kinaingiza watu: 35,696
Kilifunguliwa: 1953
Hali ya hewa: Kiwango cha juu cha joto ni 23C na cha chini 13C , uwezekano wa kunyesha mvua ni 66%
8. Uwanja utakao tumika kombe la dunia mwaka 2018
Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg
Kinaingiza watu: 68,134
Kilifunguliwa: 2017
Hali ya hewa: Kiwango cha juu cha joto ni 21C na cha chini 13C , uwezekano wa kunyesha mvua ni 60%
- Kaliningrad ni miongoni mwa kiwanja kitakachotumika hapo mwakani
Kaliningrad Stadium, Kaliningrad
Kinaingiza watu: 35,212
Kilifunguliwa: 2018
Hali ya hewa: Kiwango cha juu cha joto ni 22C na cha chini 12C , uwezekano wa kunyesha mvua ni 50%
- Uwanja wa Volgograd Arena upo umbali wa maili 585 kutoka Moscow
Volgograd Arena, Volgograd
Kinaingiza watu: 45,568
Kilifunguliwa: 2018
Hali ya hewa: Kiwango cha juu cha joto ni 28C na cha chini 16C , uwezekano wa kunyesha mvua ni 40%
- Uwanja wa Volgogrand Arena upo umbali wa maili 690
Volgograd Arena, Volgograd
Kinaingiza watu: 45,145
Kilifunguliwa: 2018
Hali ya hewa: Kiwango cha juu cha joto ni 28C na cha chini 17C , uwezekano wa kunyesha mvua ni 33%
- Uwanja wa Fisht upo pwani mwa bahari nyeusi
Fisht Stadium, Sochi
Kinaingiza watu: 47,700
Kilifunguliwa: 2013
Hali ya hewa: Kiwango cha juu cha joto ni 26C na cha chini 18C , uwezekano wa kunyesha mvua ni 40%