Afya

Hivi ndivyo Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson alivyojitangaza kuwa na virusi vya corona – Video

Hivi ndivyo Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson alivyojitangaza kuwa na virusi vya corona - Video

Bwana Johnson amekutwa na coronavirus, baada ya kufanyiwa vipimo, imesema ofisi yake Downing Street. “Nimekuwa na dalili ndogo za coronavirus, ambazo ni viwango vya juu vya joto la mwili na kikohozi ambacho hakikomi ,” Bwana Johnson amesema katika video aliyoituma kweinye ukurasa wake Twitter.

Waziri Mkuu huyo wa Uingereza amesema kuwa ataendelea kulingoza taifa kutoka nyumbani baada ya kupatikana na Covid-19.

Bwana Johnson atajitenga binafsi – katika makao yake ya kikazi ya Downing Street, baada ya kupimwa na kupataikana na virusi hivyo na muhusumu wa huduma za afya nchini Uingereza katika ofisi yake al maarufu No 10.

Boris Johnson alipimwa katika makazi yake baada ya kushauriwa na Mshauri Mkuu wa tiba wa EnglandBoris Johnson alipimwa katika makazi yake baada ya kushauriwa na Mshauri Mkuu wa tiba wa England

Bado ataendelea kuwa mkuu wa shughuli za kukabiliana na mzozo wa coronavirus, kulinga na taarifa iliyotolewa na ofisi yake.

“Ninafanyakazi kutoka nyumbani na nimejitenga. Hilo ndio jambo sahihi la kufanya”.

“Ninaweza kuendelea, nashukuru teknolojia kwamba ninaweza kuwasiliana na viongozi wakuu na kuongoza taifa dhidi ya virus.”, amesema.

” Kwa hiyo nashukuru sana kwa kila mtu anayefanya kile ninachokifanya, kufanya kazi kutoka nyumbani ili kuzuwia maambukizi ya virusi kutoka nyumba moja hadi nyingine”, aliongeza.

” Hivyo ndivyo tutakavyoshinda.”

Taarifa zaidi kuhusu coronavirus

Taarifa zaidi kuhusu coronavirus:

Bwana Johnson alipimwa katika makazi yake baada ya kushauriwa na Mshauri Mkuu wa tiba wa England, Profesa Chris Whitty, imesema ofisi yake ya Downing Street.

Haijafahamika ikiwa Bwana Johnson ataendelea kuishi na mchumba wake Carrie Symonds, ambaye ana ujauzito wa miezi kadhaa.

Mwanamfalme Charles
Mwanamfalme Charles apikutwa na coronavirus mapema wiki hii

Wanawake wajawazito wanashauriwa kuwa makini sana kuzingatia kuwa mbali na watu wengine katika jamii, na kupunguza utangamano wa kijamii kwa hadi wiki 12.

Kuna visa zaidi ya 11,600 vilivyothibitishwa vya coronavirus nchini Uingereza , na watu 578 wamekwishauawa.

Hii inakuja baada ya Mwanamfalme Charles wa Wales kukutwa na virus hivyo mapema wiki hii.

Mwanamfalme Charles, mwenye umri wa miaka 71, anaonyesha dalili ndogo “lakini vinginevyo anaendelea kuwa na afya nzuri”, alisema msemaji wake.

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents