Habari

Hivi ndivyo waziri mkuu wa Uingereza Theresa May alivyowaumbua wabunge baada ya kupiga kura ya kutokuwa na imani nae

Baada ya kupata asilimia 63 ya kura zote, sasa ana kinga ya uongozi kwa kipindi cha mwaka mmoja. Hata hivyo Waziri Mkuu May amesema pia anasikiliza mawazo ya wale waliopiga kura ya kumpinga na kuahidi kuwa atafanyakazi na vyama vyote vya siasa, kuirudisha tena nchi hiyo katika hali yake. Waziri Mkuu wa Uingereza hii leo atakabiliana na kura ya wabunge kutokuwa na imani na uongozi wake.

Wabunge wa chama tawala cha ndio waliopiga kura jana usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Mhariri wa siasa wa BBC Laura Kuenssberg anasema kucheleweshwa kwa Brexit ndiyo karata ya turufu ambayo wafuasi wa Bi May wametumia kuwashawishi wabunge wasimng’oe madarakani.

Akina nani walitaka kumng’oa Bi May?

Baadhi ya wabunge wa chama tawala cha kihafidhina wamepigia chapua kura hiyo kwa kile wanachokiamini kuwa Bi May ameshindwa kutekeleza matakwa ya wananchi walioamua kujitenga na Ulaya kwenye kura ya maoni ya mwaka 2016. Bi May alijiamini kuwa alishalituliza kundi hilo la wabunge mwezi uliopita.

Hata hivyo, hatua yake ya kuahirisha kupigiwa kura na bunge makubaliano aliyoyafikia na viongozi wengine wakuu wa EU umewapa nguvu wapinzani wake ndani ya chama. Kunahitajika uwepo wa wabunge 48 tu kati ya 315 wa chama tawala wanaotaka yeye kung’olewa ili kura hiyo iitishwe, na idadi hiyo tayari imeshavuka.

Jacob Rees-Mogg: Kwa maslahi ya taifa inabidi (Bi May) ang’oke madarakai

Jacob Rees-Mogg, ambaye amejitokeza hadharani akaitaka Bi May atoke madarakani amesema: “Mipango ya Theresa May itaiangusha serikali kama itatekelezwa. Lakini chama chetu hakiwezi kuvumilia hilo. t.

“Wabunge wa Conservative sasa inawapasa kuamua kama wanataka kwenda kwenye uchaguzi chini ya uongozi wa Bi May. Kwa maslahi ya taifa inabidi aende tu.”

Kwa nini wanataka kumng’oa?

Wabubge hao hawakubaliani na na makubaliano aliyoyaingia na EU wakiamini yataendelea kuifunga mikono Uingereza na kushindwa kujipambanua nje ya mipaka yake na duniani kwa ujumla kwa kutafuta ushirikiano bora wa kibiashara.

Hasira kali zaidi zipo kwenye mustakabali wa mpaka wa kisiwa cha Ireland chenye nchi mbili. Kusini kuna Jamuhuri ya Irelan ambayo ni mwanacha wa EU wakati Ireland ya Kaskazini ni sehemu ya Uingereza. Hivi sasa mpaka huo upo wazi lakini pale Uingereza itakapojitoa EU mpaka huo utafunguliwa na kubadili kabisa hali ya kiuchumi.

Wabunge hawataki mpaka huo kufunguliwa. Japo Bi May ameahidi kulitafutia ufumbuzi wa kudumu jambo hilo, wapinzani wake wanaamini hawezi kwa sababu viongozi wa EU wamegoma kuingia makubaliano mapya naye.

Presentational white space

Je kungekuwa na Waziri Mkuu mpya kama angeshindwa kura?

Iwapo wabunge wa chama chake wangemng’oa angesalia madarakani kwa walau wiki sita wakati chama chake kikimsaka mrithi wake.

Kama wangejitokeza wagombea wengi wabunge wa Conservative ingebidi wawapigie kura na kubaki na wawili ambao majina yao yangepigiwa kura na wanachama wa chama hicho ili kupata kiongozi mpya.

Ni muhimu kuelewa kuwa, Bi May kura ambayo angepigiwa ni ya kuvuliwa uongozi wa chama.

Ili uwe Waziri Mkuu Uingereza inabidi uwe kiongozi wa chama chenye wabunge wengi. Hivyo mrithi wa Bi May katika uongozi wa chama angekuwa Waziri Mkuu mpya bila kufanyika kwa uchaguzi mkuu.

Ili ashinde kura hiyo, na kubaki na wadhifa wake ndani ya chama na serikali, Bi May ilibidi aungwe mkono na wabunge zaidi ya nusu wa chama tawala.

Iwapo wabunge 158 kati ya 315 wa chama chake watasema wana imani naye basi atakuwa salama.

Tayari mawaziri wake wote walikuwa wameshasema kuwa wanamuunga mkono, kwa ujumla mpaka sasa kuna wabunge 158 ambao wameonesha kumuunga mkono. Hata hivyo kura hiyo ni ya siri na matokeo yanaweza kwenda upande wowote, na hivyo ni ngumu kutabiri.

Presentational white space

Nani alitazamiwa kumrithi?

Kutoka juu kushoto kwenda kulia: Jeremy Hunt, Boris Johnson, Dominic Raab, Michael Gove, Sajid Javid and Amber Rudd

Waliotajwa zaidi ni Waziri wa Mambo ya Ndani Sajid Javid, Mambo ya Nje Jeremy Hunt, Mazingira Michael Gove na waziri wa Kazi na Pensheni Amber Rudd.

Nje ya baraza la mawaziri ni waziri wa zamani Brexit Dominic Raab na David Davis na waziri wa zamani wa Mambo ya Nje Boris Johnson.

Chama cha Labour kinasemaje?

Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Labour Ian Lavery alikuwa amesema kura hiyo ni matokeo ya: “udhaifu wa Theresa May na kushindwa kabisa kuingoza serikali yake kwenye wakati muhimu kwa nchi.”

Bw Lavery pia aliongeza kuwa mabishano ndani ya chama tawala kinafanya maisha ya watu na kazi zao kuingia kwenye lindi la hatari.

Chama cha Labour kimekuwa kikipata msukumo kutoka ndani na nje kwa washirika wao wa upinzani kuitisha kura ya kutokuwa na imani na serikali ya Bi May.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents