Michezo

Hizi hapa fedha za Floyd Mayweather vs McGregor

Bondia wa Marekani, Floyd Mayweather mara kadhaa amekuwa akionyesha na kujivunia mafanikio yake aliyoyapata kupitia mchezho wa ngumi jambo ambalo limejitokeza hata Ijumaa ya wiki hii pale alipoamua kuonyesha ‘cheque’ yake ya dola za Marekani milioni 100 ambazo amejinyakulia katika pambano lake dhidi ya Conor McGregor mwaka uliyopita.

Mwezi Agosti mwaka jana, Mayweather aliingia ulingoni na kupambana na bondia Conor McGregor huko Las Vegas na kufanikiwa kuweka rekodi ya kushinda pambano lake la 50 bila kupigwa hata moja katika maisha yake ya ngumi.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Mayweather ameposti picha ya   ‘cheque’ ya milioni 100 ambayo ameshinda kutoka katika pambano lake.

Mayweather amesema “Kuna utofauti kati ya kuwa mtu smati na mwenye akili katika hali ya kawaida tu unaweza kufahamu baada ya kuweka picha hiyo.”Amesema Mayweather.

Floyd Mayweather  ameongeza kuwa katika hisabu za kawaida tu kuwa na 50 – 0, unaweza hata kusoma hii ‘cheque’ ya dola za Marekani 100,000,000.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents