Hizi ndio aina tano ya dawa za kuongeza nguvu za kiume zilizoruhusiwa na Serikali kutumika

Serikali kupitia Wizara ya Afya imezitambua rasmi aina ya dawa tano za asili baada ya kuzikagua na kujiridhisha kuwa zinatibu matatizo ya nguvu za kiume.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile

Amezitaja dawa hizo leo Machi 13, 2018, Msajili wa Baraza la Tiba za Asili na Mbadala, Dkt. Ruth Suza katika mkutano na waandishi wa habari amesema ni Ujana, Sudhi, Vatari, IH Moon na Coloidal Silver.

Dkt. Suza amesema mpaka serikali kukubali dawa hizo kutumika, walitumia kitengo cha Boring cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Mkemia Mkuu wa Serikali.

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile ametoa agizo kwa waganga wote wa tiba asili na tiba mbadala kuacha mara moja kutoa matangazo yao mbalimbali kupitia vyombo vya habari na mabango ya barabarani.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW