Michezo

Hizi ndio klabu zenye vikosi ghali zaidi duniani, Utawashangaa Arsenal na Real Madrid

Wakati klabu nyingi duniani zikitumia mamilioni ya fedha kufanya usajili ili kuendana na ushindani wa mpira wa kisasa, hatimaye klabu za soka zenye vikosi vya ghali zaidi vimetangazwa.

Kwenye orodha hiyo ya timu 50 iliyotolewa na Taasisi ya CIES Football Observatory imeonesha kuwa timu kutoka Uingereza zimeongoza kwenye 10 bora.

Kwenye nafasi ya kwanza kwenye orodha hiyo Man City imeongoza ambapo kikosi chake kina gharama ya Euro milioni  £777 ikifuatiwa na vikosi vya PSG Euro Milioni £713, Man United Euro milioni £661 na FC Barcelona Euro milioni £641 .

Katika hali ya kushangaza ni kwamba timu ambazo zinatajwa kuwa na mkwanja mrefu duniani za Real Madrid, Bayern Munich na Arsenal hazipo kwenye Tano bora ya klabu zenye vikosi ghali duniani licha ya kuingiza faida kubwa kwenye dili za matangazo, mikataba na makampuni na mauzo ya jezi.

Kwenye orodha ya vikosi ghali kwenye 10 bora Uingereza imetoa timu sita ikifuatiwa na Hispania timu mbili huku Italia na Ufaransa zikitoa timu moja moja.

Tazama orodha kamili ya timu 50 zenye vikosi ghali zaidi duniani kwa msimu huu 2017/18.

1. Manchester City – £777m

2. PSG – £713m

3. Manchester United – £661m

4. Barcelona – £641m

5. Chelsea – £524m

6. Real Madrid – £439m

7. Liverpool – £408m

8. Juventus – £396m

9. Arsenal – £356m

10. Everton – £323m

11. Bayern Munich – £321m

12. Tottenham – £316m

13. AC Milan – £269m

14 Atletico Madrid – £263m

15. Monaco – £253m

16. Borussia Dortmund – £237m

17. Roma – £231m

18. Southampton – £202m

19. Crystal Palace – £199m

20. Inter Milan – £192m

21. Napoli – £180m

22. West Ham – £157m

23. Wolfsburg – £144m

24. Leicester – £143m

25. Sevilla – £141m

26. Bayer Leverkusen – £140m

27. Stoke – £132m

28. Valencia – £130m

29. Newcastle – £128m

30. Watford – £124m

31. Lazio + Swansea £117m

33. West Brom – £115m

34. Borussia Monchengladbach – £108m

35. Schalke – £107m

36. RB Leipzig – £104m

37. Sampdoria – £100m

38. Marseille – £99m

39. Villareal – £97m

40. Fiorentina – £94m

41. Burnley – £102m

42. Lyon – £88m

43. Bournemouth – £86m

44. Torino – £83m

45. Brighton – £79m

46. Hamburg – £78m

47. Lille – £71m

48. Huddersfield – £68m

49. Sassuolo – £66m

50. Hoffenheim – £61m

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents