Burudani

Hizi ndio nyimbo 3 kutoka Afrika Mashariki anazozikubali Akothee

Msanii Akothee amezitaja nyimbo tatu anazikubali na kuzisikiliza sana kutoka Afrika Mashariki.

Muimbaji huyo wa Kenya amezitaja nyimbo hizo ni Bado ya Harmonize, Titima na Sitya Loss ya Eddy Kenzo kutoka Uganda.

“Kwanza kabisa ilikuwa ni ile ya Harmonize aliyomshirikisha Diamond, Bado. Hiyo nikishalewa tu kwenye kiti inakuwa kwenye playlist yangu inakuwa haiwezi kukosa,” Akothee amemuambia Mzazi Willy Tuva katika kipindi cha Msetoea cha Citizen Radio.

“Kwa hapa nyumbani kuna ile inaimbwa “Titima”, unajua mimi sijuagi lyrics vizuri. Uganda kuna hii ngoma yakitamb lakini naipenda ile anaitwa nani huyu Eddy Kenzo ‘Sitya Loss’,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents