Habari

Hizi ndio sababu kubwa zilizopelekea Tundu Lissu kuvuliwa ubunge, CHADEMA waja na tamko lau (+Video)

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai amesema kuwa amemuandikia barua mwenyekiti wa NEC kumtaarifu kuwa kiti cha Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki kipo wazi, kutokana na Mbunge wa jimbo hilo, Mhe. Tundu Lissu (CHADEMA) kutokuwepo bungeni bila taarifa na kutokujaza fomu ya tamko la mali na madeni.

Akitaja sababu kubwa mbili, Spika amesema ni kutotoa taarifa rasmi ya maendeleo yake, huku akionekana sehemu mbalimbali.

Sababu ya pili ni kushindwa kujaza fomu za maadili ya viongozi za Tume ya maadili, hivyo kupoteza sifa za kuwa Mbunge.

Wakati hayo yakijiri, CHADEMA nao wamepanga kutoa tamko lao kwa vyombo vya habari usiku wa leo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents