Habari

Hizi ndio sababu zinazodaiwa kusababisha ajali ya Kivuko cha Mv Nyerere Ziwa Victoria

Hizi ndio sababu zinazodaiwa kusababisha ajali ya Kivuko cha Mv Nyerere Ziwa Victoria

Kivuko cha Mv Nyerere kilichokuwa kinafanya safari zake katika ziwa Victoria kikitokea katika kijiji cha Bugorola kuelekea Ukara kilichopata ajali jana mida ya saa nane mchana, kikidaiwa kutumia masaa mawili kikiwa kwenye maji ambapo kilianza safari zake muda wa saa sita mchana.

Simanzi bado zinaendelea katika jiji hilo la Mwanza kutokana na watu kuwapoteza ndugu jamaa na marafiki kupitia ajali hiyo ya Mv Nyerere kwa inaelezwa hadi hivi sasa wamekufa zaidi ya 44 huku wengine wakiendelea kuokolewa.

kupitia mahojiano na kituo cha habari cha taifa cha TBC wananchi wa mkoa wa Mwanza wamedai Kivuko hicho  hufanya safari zake kila siku ya alhamisi katika kisiwa cha Ukerewe kikitokea maeneo ya Bugorola kuelekea Ukara na sababu za kivuko hicho kufanya safari zake siku ya alhamisi ni kwa kuwa siku ya alhamisi kunakuwa na gulio, na siku hiyo kivuko hicho hudaiwa kujaza watu wengi sana kwa uwezo wake ni kubeba abiria zaidi ya 100,lakini kabla ya ajali kivuko hicho kinadaiwa kubeba watu wengi sana.

Wakazi wa Mwanza wamelalamikia sana kitendo cha kivuko hicho kujaza watu wengi na kutokuwa na sheria yeyote ya kulinda idadi ya watu husika,lakini pia wakisema kivuko hicho hakitoshi na wamekuwa wakilalamikia serikali iweze kuongeza kivuko kingine.

Licha ya kivuko hicho cha Mv Nyerere kudaiwa kuwa kibovu na ikiwa ni miongoni mwa sababu zilizopelekea kivuko hicho kuzama lakini pia sababu,lakini mbali na hilo wananchi wengi na watumiaji wa kivuko hicho kutoka jijini Mwanza wamelalamikia sana kuhusu suala la kivuko hicho kujaza watu wengi sana na tatizo hili limekuwa kama mazoea lakini Serikali imekuwa ikijiweka mbali na malalamiko haya.

Mpaka sasa hivi ni jumla ya watu 44 walioripotiwa kufariki katika ajali ya kivuko hicho huku waokoaji wakiendelea na zoezi la uokoaji katika ziwa hilo kubwa barani Afrika Ziwa Victoria.

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents