Michezo

Hizi ndio sifa za kocha mpya wa Simba aliyemrithi Mayanja (Video)

Klabu ya soka ya Simba hii leo imemtambulisha kocha msaidizi, Irambona Masud Juma kuchukua mikoba iliyoachwa na Jackson Mayanja ambae ameamua kurudi nchini kwao Uganda.

Masud Juma sasa atasaidiana na Kocha Mkuu, Joseph Omog katika kukinoa kikosi cha Simba.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu ya Simba, Haji Manara amesema kocha, Irambona Masud Juma ni miongoni mwa walimu bora na anaelijua soka la Afrika Mashariki.

“Baada ya jana kutoa taarifa ya kumruhusu mwalimu wetu kuondoka kwenda Uganda, Klabu ya Simba leo imempokea kocha maarufu kwa watu wa soka hususani Afrika Mashariki, kabla ya kutua hapa alikuwa akiifundisha Rayon Sports ya Rwanda, amefundisha Inter  Club na Inter FC za Burundi na amecheza pia Prince Rui ya Burundi akiwa nahodha.” Amesema Manara.

Manara ameongeza “Amecheza klabu kadhaa za Rwanda ikiwemo APR, Rayon na Kiovu na kwahiyo sio mgeni kwa soka la Afrika Mashariki na pia simgeni kwa mazingira ya Tanzania mara ya mwisho alikuja wakati wa Simba Day dhidi ya Rayon.”

“Anaitwa Irambona Masud Juma yeye ndiyo atakuwa msaidizi wa kocha Joseph Omog kuanzia leo Oktoba 19.”

Katika wakati huo huo msemaji huyo wa Simba SC amemtambulisha Meneja mpya wa timu hiyo ambaye ni Richard Robert.

“Tumeboresha bench la ufundi kwa kumteuwa Meneja mpya anaitwa Richard Robert anachukua nafasi ya Dk. Cosmas Kapinga ambaye sasa amerudi kwa muajiri wake”

Kocha, Juma atasaidiana na Omog katika kipindi hiki ambacho timu hiyo inakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya mahasimu wao klabu ya Yanga Octoba 28 mwaka huu.

Sifa kubwa ya kocha huyo Mrwanda ni mtu mwenye mizuka na morali pindi awapo uwanjani hali inayowafanya wachambuzi wa soka nchini Rwanda kumfananisha na Meneja wa Chelsea, Antonio Kante au Diego Simeone wa Atletico Madrid.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents