Michezo

Hizi ndiyo Klabu Tatu zilizoshuka Daraja Ligi kuu ya Uingereza ‘EPL’ msimu huu

Ikiwa Ligi kuu ya Uingereza maarufu kama EPL inaelekea mwishoni hatimae kitendawili kigumu cha Klabu gani inashuka daraja kimeshapata jawabu.

Baada ya Wiki hii kujulikana Bingwa wa Ligi hiyo yenye msisimko zaidi Duniani kwa Chelsea kutwaa taji hilo sasa leo hii tena orodha ya Timu tatu zinazoshuka Daraja zimeshapatikana.

Klabu hizo ni Hull City ambao leo wamepoteza mchezo wao muhimu dhidi ya Crystal Palace kwa kuruhusu magoli 4-0 na kuwafanya kusalia na Pointi 34 nyuma ya Klabu ya Swansea ambao wana alama 38 na wote wakiwa na mchezo mmoja mkononi wa kufungia Ligi kiasi kwamba hata akishinda hawezi kwenda popote kwani ataishia alama 37.

Klabu nyingine zilizoshuka Daraja ni Sunderland na Middlesbrough wana alama 24 na 28 hao hata washinde mechi zao mbilizilizo salia hawawezi kuwakuta Swansea City wenye alama 38.

Mbio za kusaka nafasi ya Nne (Top Four ) bado hazina mshindi mpaka sasa ukitoa timu mbili ambazo tayari kimahesabu zimefuzu (Chelsea Bingwa na Tottenham) huku nafasi mbili zikiwindwa na Klabu ya Arsenal,Man United,Liverpool na Manchester City.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents