Tupo Nawe

Hizi ndiyo sababu tatu za Mwinyi Zahera kutojiunga na Azam FC, awaahidi wanayanga kuwaambia kila kitakachoendelea

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amefunguka mara baada ya kuhusishwa kuwa anampango wa kujiunga na Wana lamba lamba Azam FC ambao mwishoni mwa juma lililopita walimtimua mwalimu Hans Van Der Pluijm pamoja na benchi lake la ufundi.


Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera

Kupitia mahojiano yake na mtandao wa Yanga, Zahera amesema kuwa yanayosemwa hayana ukweli wowote huku akitoa sababu tatu zinazomfanya kushindwa kujiunga na matajiri hao wa jiji la Dar es salaam Azam FC.

”Mambo mengi watu wanasema kwamba kocha Zahera anakwenda Azam FC, mara viongozi wa Azam wamempigia Zahera wameshasikilizana na kufanyamakubaliano,” amesema Mwinyi Zahera.

Zahera ameongeza ”Napenda kusema hivi hii siyo mara ya kwanza watu wanaandika hivi, vitu vya hovyo na upumbavu.”

”Kwanza hakuna hata viongozi wa Azam aliyenipigia simu, pili hakuna hata kiongozi mmoja wa Azam aliyeonana na mimi na tatu viongozi wa Azam siwafahamu na hata wao wanifahamu kwa kusema rabda tumeonana wanaishia kuniona tu kwenye luninga.”

”Sasa watu wanaamka asubuhi wakishatumia vilevi wanaanza kuandika ujinga wao, napenda kuwaambia watu wote kuwa hayo ni mambo ya uongo na mimi bado ni kocha wa Yanga, ninamkataba na Yanga hakuna chochote kinachoendelea.”

”Napenda kuwasisitizia Wanayanga chochote kitakachoendelea mimi mwenyewe nitawaambia badala ya nyie kusikiliza watu wengine, hata kama nasafiri kwenda Congo nitawaambia.”

”Kuanzia leo mkisoma, kuona video au ujumbe mfupi (sms) unaosema kocha Zahera amesema hivi mujue kuwa ni uongo, msiwe na shaka yoyote na mkumbuke kocha amesema hupenda kuwaambia kitu chochote kinachofanyika kuanzia leo, mara Zahera aligombana na Kelvini Yondani mara Kelvini alitaka mshahara ni uongo na wale wanaofanya hivyo wakiona hawafanikiwi tena watachoka kufanya hivyo.”

Tetesi hizi za Zahera zimeibuka mara baada ya wikiendi hii kuibuka kwa habari iliyowashangaza watu wengi juu ya klabu ya Azam kumtimua kocha wake Mholanzi, Hans Van Der Pluijm.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW